Unordered List


KATIBU MKUU MPYA WA UMOJA WA VIJANA WA CCM(UVCCM) NDUGU RAYMOND MWANGWALA AKABIDHIWA RASMI OFISI

Aliyekuwa Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa  Ndugu Shaka Hamdu Shaka akabidhi rasmi ofisi kwa Katibu Mkuu mpya wa Umoja wa Vijana wa CCM(UVCCM) Taifa 
Ndugu Raymond S Mwangwala.

Makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi ndogo za Umoja wa Vijana wa CCM zilizopo Upanga jijini Dar es saalam.

Aliyekuwa Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Ndugu Shaka Hamdu Shaka(kulia) akikabidhi nyaraka ikiwa ni ishara ya makabidhiano ya ofisi kwa Katibu Mkuu mpya wa UVCCM Taifa Ndugu Raymond S Mwangwala(kushoto) katika ofisi ndogo za Umoja wa Vijana Upanga Dar es Saalam.
Katibu Mkuu mpya wa UVCCM Taifa Ndugu Raymond Mwangwala akiongea na watumishi wa UVCCM katika ofisi ndogo za Upanga Dar es salaam mara baada ya kukabidhiwa rasmi Ofisi.
Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Ndugu Shaka H Shaka aliyekaimu nafasi hiyo baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu UVCCM Ndugu Sixtus Mapunda kuchukua likizo ya miaka 5 kutumikia wananchi katika jimbo la Mbinga Mkoa wa Ruvuma akiwaaga watumishi wa UVCCM.

Chapisha Maoni

0 Maoni