Unordered List


DUNIA KUSHUHUDIA MKUTANO MKUBWA WA KISIASA UTAKAOFANYIKA JULAI 17 NA 18 NCHINI TANZANIA MWAKA HUU,UNARATIBIWA NA CHAMA CHA KIKOMUNISTI CHA CHINA(CPC)

  

Rais wa China  Xi Jinping.
………………………………………………………………………………. 
Rais wa China  Xi Jinping avutiwa na Umahiri wa uchapakazi wa Rais Dk. John Pombe Magufuli. 

Macho na masikio ya Dunia yanatarajiwa kujikita katika nchini Tanzania ifikapo Julai 17 hadi 18 mwaka huu.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba Tanzania imepata fursa ya kuwa mwenyeji wa mkutano mkubwa wa kidunia wa ngazi ya juu kwa vyama vilivyokuwa mstari wa mbele kupigania ukombozi kutoka kwa wakoloni katika nchi za Kusini mwa bara la Afrika.
Hivyo mkutano huo utawakutanisha wadau mbalimbali katika masuala ya siasa na uongozi  wakiwamo viongozi mashuhuri, wanasiasa wakongwe na watu maarufu.Hivyo Tanzania inatarajia kupokea ugeni mkubwa wa viongozi ambao watakuja kushiriki kwenye mkutano huo wa kidunia.
Kwa kukumbusha tu kabla ya mkutano huo kuamriwa kufanyika Tanzania kuna nchi nyingi ambazo zilikuwa nazo zinapambana kuufanikisha kuuadaa ikiwamo nchi ya Afrika Kusini lakini mwisho wa siku Tanzania ikapata nafasi ya kuandaa mkutano huo. Hii ni kutokana na utulivu, amani , upendo na mshikamano lakini zaidi ni urafiki wa kidugu na wa damu wa muda mrefu kati ya Tanzania na China.
Umahiri, uhodari na uchapa kazi wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk.John Magufuli nao umeongeza chachu na kuifanya China kuamua mkutano huo ufanyike Tanzania.

Rais wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli
Lakini pia Mifumo ya Muundo wa vyama vya CCM na CPC cha china karibu inashabihiana kwa kiwango kikubwa kwani miongozo mingi ya vyama hivi iko kwenye maandiko hakuna jambo linalofanyika ama kuamriwa katika chama  bila kufuata Katiba, Kanuni na Maadili katika vyama hivi kwa ngazi zote bila kufuata maandiko, Unaweza kuzunguka mahali pengi duniani usikute vyama vyenye Miongozo na Kanuni  na Maadili inayoongoza vyama vyao kama CCM na CPC cha China
Pongezi na shukrani ziende kwa Rais Magufuli kwa namna ambavyo utendaji kazi wake umewakuwa ukiwafurahisha mataifa makubwa mbalimbali duniani lakini pia misimamo yake katika mambo ya haki kwa Watanzania wanyonge na uzalendo wake kwa taifa kwa ujumla.
Pili pongezi kwa Watanzania wote ambao kwa namna moja au nyingine wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanaunga mkono jitihada za Rais Dk.Magufuli katika kuipeleka nchini kwenye mageuzi ya kweli ya kimaendeleo
Kutokana na Siasa zake zilizo imara duniani China imeamua kufanyia mkutano huo wenye hadhi ya kidunia chini Tanzania chini ya usimamizi na uratibu wa Chama chake cha  Kikomunisti cha (CPC) kutokana na Mahusiano ya siasa safi zilizobora kabisa kati ya nchi hizi mbili.
Nia ya CPC ni kuoenesha nia yake ya dhati ya nchi ya China katika kutaka kusaidia ustawi wa amani, umoja na Utulivu, haya ni matokeo ya nia ya dhati ya nchi hiyo kutaka kusaidia ustawi wa amani, umoja utulivu na ushitrikiano katika nchi mbalimbali.
 Kwa Tanzania ni fahari kubwa mkutano huo kufanyika nchini kwetu kwani pamoja na mambo mengine itakuwa ni fursa ya kujifunza na kupata uzoefu wa mambo mbalimbali yakiwamo ya teknolojia na  uchumi.

Baba wa Taifa la Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
China kupitia viongozi wake mahiri na wenye kuheshimika duniani ambao wanatokana na CPC wamekuwa mfano wa kuigwa katika maendeleo ya kukua kiuchimi na kulifanya Taifa hilo ndani ya miaka 73 kupiga hatua kubwa ya kimaendeleo duniani.
Hivyo uzoefu wa CPC kwenye mkutano huo utakuwa chachu kubwa inayoweza kuifanya Tanzania na nchi nyingine za Afrika kupiga hatua kubwa katika nyanja mbalimbali.
 Ni ukweli usiopingika Tanzania imetoa mchango mkubwa katika kusaidia ukombozi wa nchi mbalimbali za Kusini mwa bara la Afrika kupitia vyama vyao vya kupigania uhuru.Zikiwemo Zimbabwe (ZANU PF), Afrika Kusini (ANC), Angola (MPLA), Namibia (SWAPO) na Msumbiji (FRELIMO) Mchango ambao unakumbukwa na mataifa mbalimbali na China ikiwa miongoni mwao.
Wapigania uhuru wengi wa nchi hizo walipambana vya kutosha wakipigania kujikomboa kutoka kwa Makoloni mbalimbali yaliyotawala nchi zao ambapo wengine ama waliishi Tanzania wakijipanga na kujifunza namna ya kwenda kukomboa nchi zao ama walipitia Tanzania na kufanya mikakati namna ya kuanza mapambano huku Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na chama chake cha CCM akiwaongoza.
Mpigania Uhuru namba moja na Baba wa Taifa la Afrika Kusini Hayati Nelson Mandela
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi(CCM) na Rais wa Tanzania Dk.Magufuli kuna mambo mengi ambayo anafanya katika uongozi wake wa awamu ya tano(5) yanaivutia China. Rais Dkt Magufuli tangu aingie madarakani ametoa msimamo wa Serikali katika kuchukia na kukomesha rushwa.
Amejenga uwajibika sehemu za kazi na moja ya jambo ambalo analifanya ni namna ambavyo amedhamiria kuleta maendeleo ya Watanzania na katika hilo ameamua kuweka kauli mbiu yake ya Hapa Kazi Tu.
Sote pia tunafahamu urafiki wa miaka mingi wa muasisi wa Taifa la Tanzania Mwalimu Julius Nyerere pamoja na muasisi wa Taifa la China Mao Setung.Urafiki wa viongozi hao ulipanda mbegu inayochipua vizazi na vizazi.
Mbegu ambayo imeifanya China na Tanzania kuendelea kushirikiana na kushikamana katika kufanya maendeleo.Ni ukweli wa dhahiri China inaona Tanzania kuwa ni zaidi ya rafiki na wameendelea kuwa wamoja siku hadi siku.
Kuna miradi mingi ambayo inafanyika nchini kwetu kutokana na urafiki kati ya nchi hizo mbili. 
Hakika China ni Tanzania na Tanzania ni China.
China imekuwa rafiki wa kihistoria kwa Tanzania tangu enzi za utawala wa Serikali ya awamu ya Kwanza chini hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
Muasisi wa Taifa la China Hayati Mao Tse Tung.
Tangu awali nchi hiyo kupitia CPC ambayo ni rafiki wa karibu wa Chama Chama Mapinduzi (CCM) ilionyesha dhamira ya dhati ya kuwa rafiki anayetaka kuona Tanzania na Afrika na ikipata manufaa baada ya kukubali kutoa mkopo na kusaidia ujenzi wa Reli ya TAZARA ambayo tangu ilipoanza kutumika hadi leo imekuwa kichocheo kikubwa cha mafanikio ya kiuchumi.
Kabla ya China kukubali kujenga reli hiyo, ziliombwa baadhi ya nchi kubwa zenye maendeleo ya kiuchumi lakini zilikataa kuikopesha Tanzania na kufanikisha ujenzi wa reli hiyo.
Hatua ya China kukubali kujenga TAZARA ambayo sasa situ imekuwa kiunganishi cha mawasiliano katika ya Tanzania na Zambia, bali imekuwa pia ikitumika kusafirisha watalii na maelfu ya tani za mizigo.
China pia imekubali kujengo chuo cha “Party School” Julis Nyerere Leadership School kitakachojengwa mjini Kibaha mkoani Pwani ambacho kinatarajiwa kuwekewa jiwe la msingi hivi karibuni na Rais Dk. John Pombe Magufuli
Chuo hicho kitafundisha masuala ya Siasa, Itikadi na Uongozi ambapo nchi mbalimbali zilizopigania Uhuru kusini mwa bara la Afrika zitapata fursa ya kuleta makada wa vyama vyao na viongozi kuja kujifunza masuala ya siasa, Itikadi na Uongozi ili kuwaandaa kuwa viongozi bora katika nchi zao.

Chapisha Maoni

0 Maoni