Waziri
wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa Dr Hussein Mwinyi akiwa na baadhi
ya maafisa wa jeshi la JKT kikosi cha 841 KJ Mafinga pamoja na mkuu wa
majeshi ya JKT Tanzania Maj Gen SM Busungu wakiwa kwenye picha ya pamoja
kwenye jengo la utawala la shule ya sekondari Kawawa wakati wa uzinduzi
wa jengo hilo.
Waziri
wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa Dr Hussein Mwinyi akiwa na baadhi
ya maafisa wa jeshi la JKT kikosi cha 841 KJ Mafinga pamoja na mkuu wa
majeshi ya JKT Tanzania Maj Gen SM Busungu wakiwa kwenye picha ya pamoja
na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Kawawa iliyopo Mafinga
Mkoani Iringa.
Waziri
wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa Dr Hussein Mwinyi akiwa na baadhi
ya maafisa wa jeshi la JKT kikosi cha 841 KJ Mafinga pamoja na mkuu wa
majeshi ya JKT Tanzania Maj Gen SM Busungu wakiwa kwenye picha ya pamoja
Na hili ndio jengo la kisasa la utawala la shule ya sekondari ya kawawa lililofunguliwa na waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa Dr Hussein Mwinyi
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Waziri wa ulinzi na jeshi la
kujenga taifa Dr Hussein Mwinyi ameupongeza uongozi wa shule ya sekondari ya
Kawawa kwa ujenzi wa jengo la kisasa la utawala ambalo litachangia katika
ufanisi bora wa kazi kwa walimu na wafanyakazi wote wa shule hiyo.
Akizungumza wakati wa kuzindua
jingo hilo la utawala waziri Mwinyi alisema kuwa jingo limejengwa kwa viwango
ambavyo serikali ya awamu ya tano inataka na jingo hilo linaviwango
vinavyotakiwa.
“Kwa kweli nisiwe mchoyo wa
fadhila jingo hili limejengwa kwa kuzingatia ujenzi unaotakiwa na lina ramani
ambayo itadumu kwa miaka mingi na itakuwa auheni kwa wafanyakazi kufanya kazi
zao kwenye jingo hili” alisema Mwinyi
Waziri Mwinyi aliwataka
wafanyakzi wa shule hiyo kuhakikisha wanalitunza jingo hilo pamoja na miundo
mbinu yake kwa ajili ya vizazi vingine.
Awali akisoma risala kwa waziri
Mwingi mkuu wa shule hiyo Meja Generali Erenest Sikaponda alisema kuwa jengo
hilo la utawala limejengwa kwa shilingi 222,591,000 na kufanikiwa kuokoa kiasi
cha shilingi 103,360,000 kwa kuwa hapo awali BOQ ilikuwa inaonyesha kuwa
gharama za jengo ni shilingi 325,951,000.
Kupungua kwa gharama hizo ni
kutokana na ubunifu,matumizi mazuri ya rasilimali,nidhamu katika matumizi ya
fedha,nguvu kazi ya vijana ambao baadhi yao walikuwa mafundi na gari kubwa la
kusombea mchanga,kifusi na mawe msaada huo ulitoka katika kikosi cha 841kj
Mafinga” alisema Maj Sikaponda
Maj Sikaponda aliwashukuru
wadau mbalimbali ambao walitoa msaada wa hali na mali kusaidia ujenzi wa jengo
hilo la kisasa la utawala ambalo litakuwa msaada mkubwa kwa wafanyakazi wa
shule hiyo.
“Mheshimiwa waziri tunapenda
kuwashukuru wadau wafuata TANROAD mkoa wa Iringa kwa msaada wa kifusi cha
kujaza msingi kwa trip mia,kampuni ya kichina inayojenga barabara ya Mafinga
Igawa kwa msaada wa tripu moja ya kokoto ya ujazo wa Mita 15 za mraba,Clement
Sangale saruji mifuko 20, na Beruto Kaboda alitoa mbao 2x3 Arobain” alisema Maj
Sikaponda
Aidha Maj Sikaponda alisema
kuwa jengo hilo la kisasa la utawala linakabili na changamoto ya ukosefu wa
samani kutokana na ufinyu wa bajeti hivyo walimuomba waziri kuwasaidia kuzipata
samani hizo.
Tumalizie kwa kumshukuru mkuu
wa majeshi ya JKT Tanzania pamoja na bodi ya shule kwa usimamizi mzuri wa
mipango ya maendeleo ya shule hii.
Kwa upande wake mkuu wa majeshi
ya JKT Tanzania Maj Gen SM Busungu aliwapongeza viongozi waliosimamia ujenzi wa
jengo hilo hadi lilipofikia na kuhakikisha linajengwa kwenye ubora unaotakiwa.
Maj Gen SM Busungu alimuomba
waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa DR Mwinyi kwenda kuwaombea samani
TRA ambazo walizitaifisha kutoka bandarini ambazo maarufu kama samani za
makonda ili ziweze kutatua changamoto hiyo katika jengo hilo la utawala.
Akijibu ombi hilo la mkuu wa
majeshi ya JKT waziri Mwinyi alisema ataenda kuwaomba TRA kwa kuwa wote
wanaitumikia serikali moja.
0 Maoni