Unordered List


DC MTANDA ANOGESHA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI NKASI.



Mafunzo ya ujasiriamali kwa vitendo yamefunguliwa Leo na Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Nkasi Ndg Emmanuel Robert ambapo jumla ya VIJANA 82 walihudhuria  ambapo    MKUU wa WILAYA ya NKASI Mheshimiwa Said Mtanda aliungana pamoja na washiriki wa semina hiyo kwa kuwasisitizia wanamafunzo kushiriki katika shughuli za kiuchumi kwa kuunda vikundi vya ujasiriamali  ili waweze kujitegemea kiuchumi. 

Aidha,  Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya alibainisha namna alivyo mstari wa mbele kuwasaidia vijana wanaothubutu kujaribu kujishughulisha na alilisisitiza kuwa ataendelea kuwasaidia vijana kwa kufanya mpango ili mafunzo haya ya ujasiriamali yaliyotolewa na TAEDO chini ya Mkufunzi na MWENYEKITI wa UVCCM mkoa wa IRINGA KENANI KIHONGOSI yafanywa mpaka vijijini kata zote za wilaya ya NKASI. 

Pia DC Mtanda aliomba mafunzo hayo yapelekwe mpaka Wilaya za Kalambo na Sumbawanga Vijijini ambapo ataona namna atakavyomshawishi Mbunge wa Kalambo ili waweze kufanikisha mafunzo hayo. 
Vijana wakifuatilia mafunzo ya ujasiriamali Wilayani Nkasi yanayotolewa na Taasisi ya TAEDO

Chapisha Maoni

0 Maoni