Katibu Mkuu UVCCM Taifa Mwl Raymond Mwangwala leo amewapokea Manaibu Katibu Mkuu UVCCM Taifa ambao ni Ndg Mussa Haji Mussa (Naibu Katibu Mkuu UVCCM -Visiwani) na Ndg Galila Wabanhu (Naibu Katibu Mkuu UVCCM -Bara).
Mapokezi hayo yalifanyika Ofisi za UVCCM Makao Makuu Upanga Jijini Dar Es Salaam.
Akiongea mara baada ya kuwatambulisha mbele ya watumishi wa UVCCM Makao Makuu Mwl. Mwangwala amewatakia kazi njema za ujenzi wa Jumuiya ya Vijana huku akiwaomba watumishi, Viongozi na wana UVCCM kuwapa ushirikiano mkubwa Viongozi hao walioteuliwa na Kikao cha Kamati Kuu ya Halmshauri Kuu ya CCM Taifa.
#TukutaneKazini
#KulindaNaKujengaUjamaa
PICHANI: Kutoka Kushoto;- Ndg Hassan Bomboko (Katibu Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa, Ndg Lusekelo Nelson (Katibu Idara ya Uchumi, Uwezeshaji na Fedha UVCCM Taifa), Ndg Musa Haji Musa (Naibu Katibu Mkuu UVCCM-Visiwani), Ndg Raymond Mwangwala (Katibu Mkuu UVCCM Taifa), Ndg Galila Wabanhu (Naibu Katibu Mkuu UVCCM-Bara), Ndg Mohamed Abdalla (Katibu Idara ya Maadili na Usalama UVCCM Taifa) na Ndg Peter Kasera (Katibu Idara ya Siasa, Organaizesheni na Uhusiano wa Kimataifa UVCCM Taifa)
Katibu Mkuu UVCCM Taifa Mwl Mwangwala akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu UVCCM Taifa (Visiwani) Ndg Musa Haji Musa
Katibu Mkuu UVCCM Taifa Mwl Mwangwala akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu UVCCM Taifa (Bara) Ndg Galila Wabanhu
Watumishi wa UVCCM Ofisi ndogo ya UVCCM Makao Makuu wakiwa kwenye Picha ya pamoja na Katibu Mkuu UVCCM na Manaibu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Jijini Dar Es Salaam
0 Maoni