Unordered List


MWENYEKITI UVCCM TAIFA NDG KHERI JAMES AANZA ZIARA MKOANI NJOMBE, ASISITIZA "HESHIMA YA KIJANA NI KAZI"




Ziara ya Kikazi ya Mwenyekiti wa UVCCM TAIFA Ndg Kheri Denice James  amewasili Mkoani Njombe akitokea Mkoani Mbeya. 
Lengo la ziara ni kuimarisha jumuiya, na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2015/2020 katika mambo yanayo wahusu vijana, na kuhimiza umuhimu wa serikali na jamii kuwashirikisha na kuwawezesha vijana katika fursa za kijamii na kiuchumi.

Akizungumza na vijana wa Tarafa ya Bulongwa, Wilaya ya Makete Ndg Kheri James amewasisitiza Vijana kutambua wajibu wao kwa kushiriki kazi za maendeleo kwani Taifa lawategemea vijana zaidi "Heshima ya Kijana ni Kazi" alisisitiza Ndg Kheri James. 
Awali, akizungumza kumkaribisha Mkoani Njombe Ndg Nehemia Tweve, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Njombe aliwasihi Vijana kuitumia fursa ya ziara ya Mwenyekiti UVCCM TAIFA kujiimarisha na kuwa watekelezaji wa maelekezo watakayopata.
Mwenyekiti wa UVCCM TAIFA Ndg Kheri Denice James akisalimiana wa Viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi, Serikali, Taaaisi za Dini mara baada ya kuwasili Wilayani Makete- Njombe

BURUDANI MURUA: Ndg Kheri James akiwatunza kikundi cha Ngoma cha UVCCM Wilaya ya Ludewa

Mwenyekiti wa UVCCM TAIFA Ndugu Kheri James akisikiliza na kutoa fikra pindi alipoitembelea Hospitali ya Bulongwa

HESHIMA KWA VIJANA NI KAZI: Ndg Kheri James akizungumza na Vijana na kuwapa nini matarajio ya UVCCM 

Chapisha Maoni

0 Maoni