MNEC Theresia Mtewele akiongea na wanazuoni katika mahafali ya kwanza Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoani Njombe
Na Erasto Kidzumbe, Njombe
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (Viti 15 Bara) Bi. Theresia Mtewele amewataka wanafunzi wanaohitimu masomo wasiwe mzigo katika jamii, ameeleza kuwa elimu waliyopata ikawasaidie kutatuta changamoto katika jamii zao na kuongeza Kuwa serikali imetenga pesa Kwa ajili ya kuwezesha vijana hivyo wachangamkie fursa hiyo ili waweze kujiajiri na kujiletea maendeleo ya Kiuchumi. Ameyasema hayo katika mahafari ya kwanza ya Seneti ya vyuo na Vyuo vikuu Mkoa Njombe.
Sanjari na mahafali hiyo ndugu Mtewele ameendesha zoezi la kupokea wanachama wapya zaidi ya 150 kwa wanafunzi wa Vyuo Mkoani Njombe.
Amesisitiza wanachama na Viongozi kutofanya kosa la unafsi ili waweze kuziishi vizuri ahadi za Mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi.
Ameongeza Kuwa Kauli mbiu za "HAPA KAZI TUU" na "TUKUTANE KAZINI" zina maana kubwa sana Kwa maendeleo ya Taifa letu hivyo mtafakari na kuchukua Hatua kwani ajira ya kwanza ipo ndani ya fikra zetu. Alisema MNEC
Mwenyekiti wa Seneti Mkoa wa Njombe, Ndugu Emmanuel Mlelwa amewataka wanavyuo kuendelea Kuwa na hamasa ndani ya Chama Cha Mapinduzi na kuongeza Kuwa Kwa Siku za usoni wanataraji kuwafikia Wanafunzi wote wa Vyuo Mkoani hapo ili waweze kujiunga na CCM.
Nafarijika sana ninapo ona vijana wengi wanajiunga na CCM kwani vijana hawa wamejua mchango wa Chama cha Mapinduzi katika Taifa hili, Antony Katani Katibu wa CCM Wilaya Njombe amesema.
Naye Mbunge wa Njombe Mjini Edward Mwalongo amewaomba vijana kuwa wanachama hai wa CCM na sio kuwa wanasiasa Jina kwani siasa ni imani
"Ukiwa mwanachama wa CCM lazima uwe tayari kujitolea ili chama cha mapinduzi kiweze kujiimalisha zaidi na zaidi".
Viongozi wengine walioshiriki mahafari Hiyo ni Mwenyekiti UVCCM Mkoa wa Njombe Nehemia Tweve, Katibu Hamasa UVCCM Mkoa wa Njombe Johnson Mgimba , Mkuu wa Mafunzo UVCCM Mkoa Erasto Kidzumbe, Viongozi wa Serikali za Wanafunzi, Wakufunzi na viongozi wengine.
Mmoja ya wahitimu akikabidhiwa cheti cha kuhitimu na Mgeni Rasmi Bi. Theresia Mtewele
Pichani: Viongozi mbalimbali na Wahitimu kutoka Vyuo mbalimbali vya Mkoani Njombe wakiwa kwenye Picha ya pamoja.
0 Maoni