
Taifa Stars wamefanikiwa kutinga ya mwisho ya mchujo baada ya ushindi wa penalti 4-1 dhidi ya Kenya jioni ya leo Uwanja wa Moi Kasarani mjini Nairobi, Kenya.
Katika mchezo wa kwanza, uliochezwa Jijini Dar es Salaam Timu hizo zilishindwa kufungana na kutoshana nguvu ya 0-0.
Mchezo wa pili uliweza kumalizika kwa dakika 90 bila kufungana na kwenda kwenye hatua ya matuta na kipa mkongwe, Juma Kaseja aliweza kuwa shujaa owa kuokoa penati ya Michael Kibwage.
Kipa huyo amerejeshwa kikosini baada ya miaka sita na kuendelea kudhihirisha ubora wake.Kwa upande wa Tanzania Waliopata penati ni mabeki Erasto Nyoni, Paul Godfrey ‘Boxer’, Gardiel Michael na mshambuliaji Salum Aiyee.
Kenya walipata penalti moja tu, ambayo ilifungwa na Cliffton Miheso Ayisi, huku nyingine wakikosa Michael Kibwage na Joash Achieng Onyango.
Sasa Tanzania itakutana na Sudan katika hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania tiketi ya CHAN ya mwakani nchini Cameroon, mechi ya kwanza ikichezwa Dar es Salaam Septemba 20 na marudiano Oktoba 18 Khartoum.
Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Juma Kaseja, Paul Godfrey, Gardiel Michael, Erasto Nyoni, Kelvin Yondan, Jonas Mkude, Frank Domayo/Salim Aiyee, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, John Bocco/Ayoub Lyanga, Iddi Suleiman ‘Nado’ na Hassan Dilunga/Abdulaziz Makame.
Kenya; John Oyemba, Philemon Otieno/Ibrahim Shambi, Cliffton Miheso, Mike Kibwage, Joash Onyango, Dennis Odhiambo, Samuel Onyango, Kenneth Muguna, Sydney Lokale/Enosh Ochieng, Whyvone Isuza na Duke Abuya/ David Owino.
0 Maoni