Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa Wa Kilimanjaro Umeongoza Ibada ya Shukrani Kwa Mwenyezi Mungu Kwa Kushirikisha Viongozi Wa Dini Zote Katika Viwanja Vya CCM Wilaya ya Siha Vilivyopo Katika Wilaya Ya Siha.
"Nawashukuru Sana Viongozi Wa Dini Kwa Kuitikia Wito Huu Kufika Mahai Hapa Na Tunafanikiwa Katika Swala Hili La Kuliombea Taifa Letu Tanzania. "Ivan Moshi Mwenyekiti Uvccm (M) Kilimanjaro
Ukisoma Mambo Ya Nyakati 2 Mlango Wa 7.14 Unasema "Ikiwa Watu Wangu Walio Itwa Kwa Jina Langu Watajinyenyekesha Na Kuomba Na Kunitafutia Na Kuziacha Njia Zao Mbaya Basi Nitasikia Toka Mbinguni Na Kuwasamehe Zambi Zao Zote Na Kuponya Nchi Ya Kwao",Rais wa JMT Alikuwa Anayo Sababu Katika Kuruhusu Taifa Liingie Katika Maombi."Ivan Moshi Mwenyekiti Uvccm (M)Kilimanjaro.
"Wanasema Mfalme Mzuri Ni Yule Anayemuamini MUNGU Na Hili Tunampongeza Rais Wetu Wa JMT Dr John Pombe Magufuli Kwa Kuonesha Msimamo Wake Kuhusu Swala La IMANi."Ivan Mosha Mwenyekiti Uvccm (M) Kilimanjaro.
"Tunakila Sababu Ya Kumshukuru MWENYEZIMUNGU Kutuepusha Na Janga La Corona , Ndani ya Taifa Letu Na Ndio Maana Sisi Kama Uvccm Mkoa Wa Kilimanjaro Leo Tumekutana Hapa Kwa Lengo, Nia Ya Kumshukuru Mungu na Kuendelea Atuepushe Na Janga Hili La Corona." Asia Hamlaga Katibu Uvccm (M) Kilimanjaro.
"Wote Tunajua Hali Zetu Lakini Mh Rais Wetu Ajatufungia Ndani (LockDown) Ametuacha Wananchi Tufanye Kazi " Asia Hamlaga Katibu Uvccm (M) Kilimanjaro.
"Tuendele Kumshukuru Rais Wetu Wa JMT Kwa Namna Alivyo Simama Imara Juu Ya Kupambana Na Janga Hili Na Leo Tunaona Mataifa Makubwa Yanaiga Nchi Yetu Ya Tanzania Namna Tunavyopambana Na Janga Hili la Corona"Asia Hamlaga Katibu Uvccm(M) Kilimanjaro.
Aidha Mkuu Wa Wilaya ya Siha Alisema Yafuatayo
"Tumekuwa Nchi Ya Kuigwa Na Mataifa Makubwa Yaliyoamini Katika Technologia Kuliko Kuamini Katika MUNGU Na Mmeona Jinsi Ambayo Yametahabika Juu ya Janga Hili la Corona"Mh Onesmo Buswelu Mkuu wa Wilaya ya Siha Katika Ibada Ya Shukrani Kwa Taifa.
"Tumekuwa Nchi Ya Kuigwa Na Mataifa Makubwa Yaliyoamini Katika Technologia Kuliko Kuamini Katika MUNGU Na Mmeona Jinsi Ambayo Yametahabika Juu ya Janga Hili la Corona"Mh Onesmo Buswelu Mkuu wa Wilaya ya Siha Katika Ibada Ya Shukrani Kwa Taifa.
"Historia Inaonesha Katika Vitabu Vya Dini Kwamba Hakuna Vita Ambayo Taifa Limeshinda Bila Kumtanguliza Mungu , Tunafundiahwa na Tunasoma Taifa La Israel Hakuna Siku Walishinda Vita Walipomuacha MUNGU Lakini Kila Walipo Rejea Wakamtazama MUNGU Wao Wanao Muabudu Aliwanusuru Na Unandqmizwaji Wa Maadui" Mh Onesmo Buswelu Mkuu wa Wilaya Ya Siha Katika Ibada Ya Shukrani Kwa Taifa.
Vitabu Vinasema " Nabii Musa Alipokuwa Kwenye Safari Ya Kutoka Misri Kwenda Canan Aliiona Canan Lakini Akuifikia Lakini Alipotazama Canan Akawaambia Mtazameni MUNGU Akawatazamisha Israel Kwa MUNGU Kwanza Na Sisi Rais Wa JMT Dr John Pombe Magufuli Alituambia MUNGU KWANZA Na Ndio Maana Tumepata Mafanikio Makubwa Juu Ya Kupamabana Na Janga Hili La Corona."Mh Onesmo Buswelu Mkuu wa Wilaya ya Siha Katika Ibada ya Shukrani Kwa Taifa.
Ibada Hii ya Shukurani Kwa iliongozwa Na Viongozi wa Madhehebu ya Dini Zote kwa Waumini Wote na Kuhudhuliwa na Wajumbue Wa Kamati ya Uvccm Mkoa Kilimanjaro, Wajumbe wa Baraza Uvccm Mkoa wa Kilimanjaro, Kamati ya Siasa Wilaya ya Siha, Kamati ya Utekelezaji Uvccm Wilaya ya Siha , Mganga Mkuu Wilaya ya Siha na Wadau Mbali Mbali.
Tunaungana na Rais Wetu Kurudisha Shukrani Kwa MWENYEZI MUNGU
Imetolewa na;
Idara ya Hamasa Mkoa Wa Kilimanjaro.
Idara ya Hamasa Mkoa Wa Kilimanjaro.
![](https://uvccm.co.tz/wp-content/uploads/2020/05/690E6436-6C71-4339-A472-8063298972B1-300x169.jpeg)
![](https://uvccm.co.tz/wp-content/uploads/2020/05/5E86210E-6EB8-47D8-A9B6-4566C14032B2-300x169.jpeg)
![](https://uvccm.co.tz/wp-content/uploads/2020/05/B1E8225E-303D-40B7-9A69-B641BCAE34ED-300x200.jpeg)
![](https://uvccm.co.tz/wp-content/uploads/2020/05/2F4A0550-D050-449C-BD0C-DD0DFB695E30-300x169.jpeg)
![](https://uvccm.co.tz/wp-content/uploads/2020/05/7E171B16-6E17-4E9C-8928-9DB9E809197C-300x200.jpeg)
![](https://uvccm.co.tz/wp-content/uploads/2020/05/4FC20243-1FD4-427C-BAB1-7F005BADA14C-300x244.jpeg)
![](https://uvccm.co.tz/wp-content/uploads/2020/05/B1E8225E-303D-40B7-9A69-B641BCAE34ED-300x200.jpeg)
0 Maoni