Makamu wa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa TanzanIa Mhe Samia Suluhu Hassan amekua Mgeni rasmi katika Kongamano lililoandaliwa na Tawi la Chuo kikuu Cha UDSM la Kumpongeza Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2015-2020.
Wakizungumza Viongozi wa Tawi hilo wametoa Pongezi kwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwasaidia watoto wa wanyonge na Masikini kupata mikopo ili kuweza kuendelea na Masomo yao.
Pia Viongozi hao wametoa pongezi kwa Rais Magufuli kwa hatua mbalimbali alizochukua kutokana na Kulikabili gonjwa la Corona nchini.
Akizungumza katika Kongamano hilo Mhe Mama Samia Suluhu ameupongeza Umoja wa Vijana Wa CCM kwa kazi ya kuijenga Jumuiya kwanzia katika matawi wanayoifanya ya kuendelea kuhamasisha Vijana Kuzidi kuunga Mkono Chama Cha Mapinduzi .
Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Taifa Komred Kheri Denis James (MCC) ametoa pongezi nyingi kwa namna vijana wanavyosimama imara na kuhakikisha wanakijengea chama na Taifa na kuwahasa kuelekea Uchaguzi huu kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za Ubunge na Udiwani sambamba na kuhakikisha kuwa Chama Kinashinda katika Ngazi zote.
Kongamano hilo limehudhuliwa na viongozi na Wajumbe wa kamati za Siasa za Wilaya na Mkoa wa Dar es salaam wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar Es Salaam Bi Cathy Kamba.
#TukutaneKazini
0 Maoni