Kamati ya Utekelezaji ya Uvccm Mkoa wa Ruvuma ikiongozwa na Mwenyekiti wa Uvccm Comredi Raymund Mhenga wamefanya ziara wilaya ya Nyasa na kuzungumza na Vijana kuhusu maandalizi ya Uchaguzi mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani.
Sambamba na hilo kamati ya utekelezaji ya Uvccm Mkoa wa Ruvuma iliweza kutembelea Eneo la ujenzi wa Nyumba ya Katibu wa Uvccm Wilaya hiyo na kufurahishwa na maandalizi ya ujenzi wa nyumba hiyo ambao utaanza mapema tarehe 26/06/2020.Mwenyekiti alimshukuru Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Bi Isabela Chilumba kwa kuichangia Jumuiya Tofali kwa Ajili ya ujenzi na Ramani ya Nyumba hiyo sambamba na kuhaidi support kubwa kuhakikisha Nyumba hiyo inakamilika.
Pia kamati ya utekelezaji iliweza tembelea kijiji cha Kigongo na kutoa cement kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya Tawi kama walivyohaidi kwenye ziara iliyopita na Pia kutoa Vifaa vya michezo Mjini Mbambabay kwa Vijana walioshiriki Mechi maalumu ya kumpongeza Mh Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa Kazi kubwa ya utekelezaji wa Ilani.
*Imetolewa na Idara ya Uenezi
*UVCCM Mkoa wa Ruvuma
0 Maoni