Unordered List


MGOMBEA URAIS CCM DKT JOHN POMBE MAGUFULI AAHIDI MAKUBWA MKOA WA SHINYANGA

 

Na. Said Mwishehe,Michuzi TV-Shinyanga

MIKUTANO ya Kampeni ya Uchaguzi Mkuu ya Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.John Magufuli imeendelea kuleta matumaini makubwa ya maendeleo ya wananchi ambapo mgombea urais huyo akiwa mkoani Shinyanga ameeleza jinsi Ilani ya Uchaguzi ilivyoanisha maendeleo yanayokwenda kufanyika mkoani humo baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu mwaka huu.

Dk.Magufuli ametumia muda mwingi leo Septemba 3,2020 kuzungumza na maelfu ya wananchi wa Shinyanga waliofika kumsikiliza katika mkutano wake wa kuomba kura ambapo ameelezea Ilani ya CCM imetaja miradi ya maendeleo  inayokwenda kutekelezwa iwapo Chama chake kitapata ridhaa ya kuongoza tena kwa miaka mitano.

Akiwa Uwanja wa Kambarage uliopo Shinyanga Mjini, Dk.Magufuli amesema katika mkoa huo kuna maendeleo makubwa yamefanyika chini ya Serikali ya Awamu ya Tano na kwamba mwaka 2015 walimuamini na kunichagua awe Rais, amefarijika kipindi cha miaka mitano ameshirikiana  nao kufanya mambo mbalimbali yakiwemo ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa fedha ambayo ujenzi wake unaendelea. Pia ujenzi wa hospitali za Wilaya katika mkoa huo ambapo Sh. bilioni 3.6
 
Amesema katika sekta ya dawa nako Sh.bilioni 16 zimetumika huku Serikali kali ikiajiri watumishi wengine wapya kwa ajili ya kuendelea kuboresha huduma za afya katika Mkoa wa Shinyanga.Jumla ya Sh.bilioni 31.9 zimetumika kwa ajili ya maendeleo ya mkoa huo

Pia amezungumzia jinsi ambavyo Serikali imeboresha miundombinu ya barabara kwa kuweka lami katika baadhi ya barabara ambazo nyingine ujenzi unaendelea, kuimarisha usalama wa watumia barabara kwa kuweka taa.Kuhusu amesema kilimo na mifugo yapo yaliyofanyika mengi ukiondoa kusamehe kodi 104, Serikali imeendelea kuboresha miundombinu, imetoa chanjo, imejenga machinjio na katika Uchaguzi Mkuu uliopita viwanda ilikuwa moja ya ahadi kubwa na ujenzi wa viwanda umefanyika na unaendelea.

"Sisi Chama Cha Mapinduzi tumekuja na ahadi ambazo ziko kwenye Ilani yetu na ndio ambayo Rais,Wabunge na Madiwani watatakiwa kuyatekeleza. Kwa Shinyanga ukurasa wa  31 unazungumzai kuimarisha vyama vya ushirika, shinyanga kulikuwa na vyama vya ushirika na tunataka vyama hivyo viende kwa spidi kama ile ya zamani.Ukurasa wa 35 unazungumzia wa magharala na vihenge vya kisasa.

"Ukienda ukurasa 44 unazungumzia juu ya kujenga vituo vya kuchakata na kuhifadhi mazao katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo ya Arusha, Mwanza Tabota, Morogoro,Mtwara,Singida Songwe Tanga na mikoa mingine kadhaa na Shinyanga ikiwemo.Kwa hiyo kwa hiyo nikieleza katika kipindi kingine cha miaka mitano tutajenda viwanda vya nyama na tunamaanisha,"amesema Dk.Magufuli wakati anafafanua baadhi ya kurasa za ilani hiyo.

Pia amesema katika Ilani hiyo ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2020 , ukurasa wa 45 unazungumzia kuchakata mazao ya kilimo na Shinyanga ni wakulima wazuri wa kilimo cha pamba.Ukurasa wa 51 unazungumzia kuongeza uzalishaji wa mazao yatokana na pamba.Mengi yameanishwa hata ufugaji samaki wameahidi kuendelea kujenga mabwawa makubwa.Ukurasa wa 77 unazungumzia ujenzi wa barabara ya kutoka Kagongwa ,Bukoba hadi Kahama yenye urefu wa kilometa 31.

 "Yapo mengi midradi ya REA yapo ukurasa wa 94.Ilani imezungumzia ujenzi wa reli ya treni ya kisasa inayotumia umeme inayotoka Makotopola,Tabora na Tabora hadi Isaka mpaka Mwanza yenye urefu wa kilometa 250 na fedha zinazotumika ni matrilioni ya fedha.Mtakaonufaika na miradi hii ni vijana na hiyo ndio ya njia ya kutengeneza ajira, ajira ni pamoja na miumdombinu imara ambapowananchi watashiriki kwenye shughuli za uchumi

"Mwezi wa Nane au wa Tisa kabla ya kumalizika kwa mwaka huu ujenzi wa reli hiyo  utaanza.Ukusara 95 unazungumzia tena viwanja vya ndege. umetoa ufafanuzi wa ndani zaidi, lakini ukurasa wa  99 unazungumzia umeme imara, tumesema nchi yetu iwe na umeme wa kutosha na tutakapomaliza mradi wa Bwawa la kufua umeme la Nyererere tutakuwa na umeme wa kutosha na kama unavyosema tutakuwa kama Ulaya.

"Pia tutakamilisha utekelezaji wa awamu ya pili ya njia ya umeme ya kutoka Iringa, Dodoma,Singida hadi Shinyanga.Ukurasa wa 105  unazungumzia madini , yako mengi yamezungumza nitasoma machache, itakuwa ni kuimarisha mifumo ya kisheria na kisera, tunataka madini yanufaishe wananchi wa kawaida , ndio maana tunataka madini haya yachimbwe na wananchi wenyewe.

"Tutaendelea kuimarisha maeneo ya uchimbaji madini, mikopo na teknolojia ili kurahisisha uchimbaji na hayo yameendelea kufafanuliwa katika ukurasa wa 105 ,106, 107 ,11.Tunazungumzia maliasili katika mpango wa miji na majiji .Ukurasa 118 kuwawezesha wananchi.
 
katika mikoa mbalimbali na Shinyanga nayo imo,"amesema Dk.Magufuli mbele ya maelfu ya wananchi wa Mkoa huo.Karibia kila ukurasa wa Ilani yetu unazungumzia maendeleo na Shinyanga nayo imo."



 
Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Shinyanga mjini katika Mkutano wa Kampeni za Urais kwa upande wa CCM uliofanyika katika uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga leo tarehe 03 Septemba 2020.

 
Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza huku akiwa ameishika Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM kwa mwaka 2020-2025 katika mkutano wa Kampeni za Urais kwa upande wa CCM uliofanyika katika uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga leo tarehe 03 Septemba 2020.


Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa anafurahia wakati akiangalia msanii wa Singeli Sholo Mwamba alipokuwa akitumbuiza katika uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga. 



Sehemu ya Wananchi wa Shinyanga wakishangilia wakati Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akizungumza katika mkutano wa Kampeni Shinyanga mjini. 

Chapisha Maoni

0 Maoni