Unordered List


TANZIA YA CCM KUFUATIA VIFO VYA VIONGOZI WAKE.


                         TANZIA:


Chama Cha Mapinduzi kimepokea kwa masikitiko na huzuni kubwa taarifa ya kifo cha Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kutoka Mkoa wa Morogoro Ndugu Hassan Masoud Mamba (Bantu) kilichotokea Hospitali ya Taifa Muhimbili tarehe 18 Mei 2021 na kifo cha  Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Tabora Ndugu Mwajuma Muhina kilichokea katika Hospitali ya Wilaya Nzega tarehe 18 Mei 2021.


Mwenyekiti  wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan amevitaja kwa pamoja vifo hivyo kuwa ni msiba mzito kwa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake. Kuwapoteza viongozi hao wawili ambapo Chama kiliwategemea, kuwatumaini na kunufaika nao kwani walikuwa wanasiasa hodari, wazoefu na wachapakazi.


"Kazi ya Mwenyezimungu haina makosa, kupoteza kwao maisha wakati huu ni jambo la kusikitisha kwani ni wakati ambao ushauri wao, upeo na maarifa waliyokuwa nayo katika kufanikisha kazi na mipango ya kisiasa, kioganaizesheni na kisera ilikuwa ni msaada mkubwa kwa Chama Cha Mapinduzi"- Ndugu Samia Suluhu Hassan.


Chama Cha Mapinduzi kinatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wanachana wa CCM Mkoa wa Morogoro na Tabora kwa kuwapoteza Viongozi wetu wapendwa. Tunawaomba kuwa na uvumilivu, ustahamilivu na subira kwenye kipindi hiki kigumu cha maombolezo na mazishi.


 Hakika Sisi ni wa MwenyeziMungu na Kwake ni Marejeo Yetu. 


Imetolewa na;



Shaka Hamdu Shaka 

Katibu  wa Halmashauri Kuu ya Taifa

Idara ya Itikadi na Uenezi.

19 Mei 2021.

 

 Pichani ni Marehemu Mwajuma Muhina aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Tabora  kabla ya kifo chake .

 Pichani ni Marehemu Hassan Masoud Mamba (Bantu) aliyekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kutoka Mkoa wa Morogoro kabla ya kifo chake.

Chapisha Maoni

0 Maoni