Unordered List


TAMKO rasmi la Ndugu Zitto Z. KABWE (MB) kuhusiana na kinachoitwa “Taarifa ya Siri ya Chadema”

 Siku chache zilizopita Taarifa Ya Siri ya Chadema ilikuwa imesambaa sana Mitandaoni ikielezea Mengi sana kumuhusu Mh. Zitto kwa Kuwasaliti wenzake ktk Chama, Lakini Jana Zitto kavunja ukimya wake kwa Kutoa Taarifa kwa Watanzania, Soma hii.......!!!

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAMKO rasmi la Ndugu Zitto Z. KABWE (MB) kuhusiana na kinachoitwa “Taarifa ya Siri ya Chadema”
"Ndugu Wanahabari,
NILIPOKUWA katika ziara ya bara la Ulaya kati ya Oktoba 21 mpaka Novemba 2 mwaka huu (2013), nilipokea kwa njia ya barua pepe ripoti inayoitwa “Taarifa ya Siri ya Chadema” ambayo pia ilikuwa imesambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii.
“Taarifa ya Chadema inasema kwamba chama hicho (chama changu) kilikuwa kimechunguza mwenendo wangu tangu mwaka 2008 hadi 2010 na kubaini kuwa mimi napokea fedha kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuivuruga Chadema.
Ripoti hiyo ilinihusisha pia na mwananchi raia wa Ujerumani, Andrea Cordes ambaye, kwa mujibu wa ripoti hiyo, alinisaidia kupokea na kuhifadhi kiasi cha dola 250,000 za Marekani kupitia kwenye akaunti yake binafsi.
Taarifa hii ya kutunga na iliyojaa uongo wa kiwango cha kutisha, imenifadhaisha, kunisikitisha na kunikasirisha.
Taarifa hii iliibuliwa katika kipindi ambacho nilikuwa safarini kutetea haki za Watanzania na Waafrika ambao utajiri wao wa rasilimali unafaidiwa na watu wachache waliohifadhi mali katika nchi za nje na pia kupigania makampuni ya mataifa tajiri yalipe kodi stahiki katika nchi zetu.
Pengine lengo la ripoti hiyo lilikuwa ni kutaka kunipoteza kutoka katika nia na dhamira yangu ya dhati ya kutaka Watanzania wafaidike na utajiri wao. Muda ambao watunzi wa ripoti hiyo waliamua kutoa taarifa yao unazua maswali mengi kuliko majibu.
Nafahamu kwamba mimi ni mwanasiasa ambaye nimekuwa mlengwa (target) wa mashambulizi kutoka kwa makundi mbalimbali ya wanasiasa na vikundi vyao. Kama mwanasiasa, niko tayari kupokea changamoto zozote zinazokuja na uanasiasa wangu.
Hata hivyo, ambacho sitakubali ni kwa watu kutumia jina langu na uanasiasa wangu kunichafua mimi binafsi na watu wengine wasiohusika kwa sababu ya kutaka kutimiza malengo yao ya kidhalimu.
Raia huyo wa Kijerumani tayari amekana kuhifadhi fedha zangu. Kwa maelezo yake kwa baadhi ya viongozi wa Chadema amekana kuwa na akaunti inayotajwa na amekana pia kuwepo nchini Ujerumani katika siku na wakati uliotajwa kwenye ripoti hiyo.
Ripoti hiyo imemtaja pia mtu kama Dk. Charles Kimei, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB ikidai kwamba nilikutana naye na alishiriki kwenye igizo hilo la kunipa fedha.
Niseme mapema kwamba tangu kuzaliwa kwangu sijawahi hata mara moja kukutana na Dk. Kimei popote pale ndani au nje ya nchi. Kumuingiza mtu ambaye amejenga jina lake kwenye taaluma ya kibenki kwa sababu tu ya lengo ovu la kumchafua Zitto Zuberi Kabwe si uungwana bali ni unyama.
Kutokana na uchafuzi huu wa wazi dhidi ya taswira yangu binafsi na watu wengine walioingizwa kwenye mkumbo huu, nimeandika rasmi kwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.Wilbrod Slaa kumwomba athibitishe kwamba kinachoitwa Taarifa ya Siri ya Chadema ni kweli ni taarifa ya chama au kiikanushe ili niweze kuchukua hatua za kisheria dhidi ya waandishi wa hekaya hiyo.
Cha ajabu, nimepokea ujumbe wa kutishiwa maisha kutoka kwa mtu anayejiita Theo Mutahaba na kuahidiwa KUPOTEZWA endapo nitaendelea na jitihada zangu za kupambana na ufisadi na kutafuta haki kwa Watanzania wote pasipo kujali tofauti zao za kiitikadi, kikanda, kikabila na kidini.
Natarajia kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wote ambao wamehusika na utungaji na uenezi wa taarifa hii. Nitahakikisha kwamba wahusika wanatafutwa na kufunguliwa mashitaka stahiki ya upotoshaji na kuchafuana.
Ni matarajio yangu kwamba wale wenye mapenzi mema na Tanzania, mimi binafsi na utawala wa sheria, wataelewa nia yangu ya kutafuta haki katika suala hili.
Nimeamua kujitolea maisha yangu kwa ajili ya Watanzania na kama alivyopata kusema Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela; “Struggle Is My Life.”
Forward Ever, Backward Never- Kwame Nkrumah
Zitto Kabwe (Mb)
10/11/2013"
 
Katika pita pita zangu kuifatilia Habari hii Nikakuta haya Mitandaoni. na  JAMII FORUM.
--------------------------------

------------------------------------
Malalamiko ya Andrea Cordes kwa mhusika Kupitia Twitter








--------------------------------------------------

Barua ya malalamiko ya Andrea Cordes kwenda CHADEMA
Dear Hon. Dr. Slaa,

Dear Hon. Mbowe,
Dear Hon. Mnyika,




With great disappointment I got to learn that members of your party are spreading lies about my person.
A report with the title "RIPOTI YA SIRI JUU YA ZITTO KABWE" of November 4th, which indicates that it is by CHADEMA headquarters *Nyaraka hii imechomolewa kwa siri toka Chadema makao makuu*, was first published in parts in the Internet platform "Jamii Forum" on the weekend of the 26th of October 2013.
After bringing my complaint towards the owner of Jamii Forum the threads got deleted.


On the morning of the 6th of November 2013 the address of a created blog with the report was publically circulated by Mr. Yericko Nyerere via Twitter. The blog address http://halihalisi255.wordpress.com/2...a-zitto-kabwe/ only contained the above mentioned report.


The report mentions me as a person to be involved in corrupt activities with your Deputy Secretary General Hon. Zitto Kabwe. It has indicated my private telephone number and the place where I am working.
This defamation of my person is not acceptable.



I have reacted on the 6th of November by mentioning several facts to refute the report. Please find these tweets in the attachment. The tweets were mentioned towards Mr. Yericko Nyerere, who pretends to be a member of your party, to Hon. Kabwe and to Hon. Mnyika.


After my reaction the report was deleted in the evening of the 6th of November from the blog.
The deletion thus does not resolve the problem that a report which indicates to be from your party has tried to slander my name in the public. Moreover bringing my workplace into the game and therefore putting my organization in a wrong light and even bringing my appointment with this organization in danger.


I therefore request you to take necessary actions to recover my name in the Tanzanian public.
CHADEMA has to dismiss this report as not being written by the party but by an individual who intends to defaming one of your party leaders.
If CHADEMA will not dismiss the parts of the report which mention my person then I kindly ask you to bring forward the proofs against me that I can accordingly refute them with the necessary actions.


I am awaiting a statement and clear position by your party to recover my name and to take necessary actions to take the authors of this report to court.


My organization and lawyer are informed about the slander campaign in regard to my person. Accordingly legal actions will be taken if CHADEMA will not refute the report officially and bring justice to the people affected from it.


With warm regards
Andrea Cordes



--
Andrea Cordes
Member of the SPD
Majibu ya ndugu John Mnyika kwa niaba ya CHADEMA kwa Andres Cordes




*Copy za barua kwa hisani ya members wa JamiiForums - Zimehakikiwa na Ndugu Zitto Kabwe kuwa ni nakala za kweli, Ruhusa ya kuziweka public zimetoka kwa Andrea Cordes.

Chapisha Maoni

0 Maoni