Jumamosi, 29 Oktoba 2016

MKUU WA WILAYA YA KONGWA MH NDEJEMBI AZINDUA KAMPENI YA ONDOA NJAA KONGWA (ONJAKO)

Mkuu wa wilaya ya Kongwa Mh Deo Ndejembi ameanzisha kampeni ya kuondoa Njaa wilaya ya Kongwa, (ONJAKO)
Kampeni ambayo itakuwa nikwaajili ya msimu wa Mwaka 2016/2017 na Endelevu kwa Miaka 5.
Mkakati huu unamalengo mahususi ili kukabiliana na Hali ya Ukame.
Kutokana na hayo DC Ndejembi ameagiza kuwa na kilimo cha Mtama zaidi kuliko Mahindi. Kwani Wilaya ya Kongwa ina Kaya 59141, na kila kaya kama ikilima Heka mbili (2) za Mtama, Mavuno itakuwa Tani 71000, za Mtama sawa na 83% ya hitaji la chakula Wilayani Kongwa.
Kutokana na hayo kuna uhitaji wa mazao mengine pia kulingana na maeneo husika.
1. Kuongeza uzalishaji wa mtama toka tani 1/ Hekta mwaka 2016 hadi tani3/hekta ifikapo june 2021,
2. Kuongeza Uzalishaji wa Muhogo mbichi toka tani 6/hekta Mwaka 2016 hadi tani 10 hekta  mwaka 2029
3. Kuongeza uzalishaji wa Alizeti toka tani 1.2/ hekta mwaka 2016 hadi tani 1.8/hekta mwaka 2021
4. Kuongeza uzalishaji wa ufuta toka tani 0.5/hekta mwaka 2016 hadi tani 1.2/hekta ifikapo june 2021
5. Kuongeza pato la Mtu/watu toka Tsh 500,000/= Mwaka 2016 hadi Tsh 800,000/= June 2021.
Akizungumza na Madiwani, Watendaji wa Kata zote 22, Maafisa Tarafa zote 3, Waratibu Elimu Kata, Wenyeviti wa Vijiji vyote 87 vya Wilaya ya kongwa na watendaji wao, pamoja na wadau waalikwa na Kilimo.
 Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Ndenjembi akizungumza katika Uzinduzi wa kampeni ya Ondoa njaa Kongwa (ONJAKO).
   Katika Uzinduzi wa Kampeni hiyo Mhe DC Ndejembi kawaagiza kuwa ufanywe utaratibu wa kuhakikisha kila kaya inalima Heka zisizopungua mbili (2) za Mtama, Mbili za Mahindi, kulingana na eneo husika wakishauriwa na maafisa ugani lakini mtama ni lazima kwa kila kaya hata kama analima mahindi nakwa vijana wote wasio na kazi wilayani Kongwa wapewe Hekali mbili mbili ili waache kucheza pool table.
pia katika uzinduzi huo Mhe Ndejembi Ameagiza  kuanzia Leo  Marufuku kucheza Pool Table mpaka ifikapo Jioni ya Saa 10, na atakaekaidi hilo sheria stahiki zitachukuliwa.


Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu