Jumapili, 8 Januari 2017

MATEMBEZI YA UVCCM ZANZIBAR KUELEKEA KILELE CHA MIAKA 53 YA MAPINDUZI ZANZIBAR YAZIDI KUFANA


Matembezi ya Vijana Uvccm Zanzibar kuelekea katika kilele cha Kuazimisha Sherehe za miaka 53 Ya Mapinduzi ya Zanzibar Yazidi kuwa ya aina yake

Mapema ya leo Naibu Katibu Mkuu Uvccm Zanzibar Ndg:Abdulghafari Idrissa ameongoza zaidi ya Vijana 500 toka Tanzania bara na Visiwani kuendelea na matembezi ya hiari yenye kauli Mbiu,
"ASIYE YAENZI MAPINDUZI NI ADUI WA MAENDELEO YA WAZANZIBAR".
Matembezi haya alianzia katika Skuli ya Machui kwa Shughuli ya Ujenzi wa Taifa kuchimba Msingi wa kuongeza Madarasa.

 Mara baada ya kukamilika kwa Shughuli ya Ujenzi wa Taifa Msafara wa Matembezi yalielekea kijiji cha Mwera ambako matembezi hayo yamepokelewa na Viongozi wa Chama na Serikali katika Mkoa wa Magharib.

Ndani ya Mkoa wa Magharib Naibu Katibu Mkuu Uvccm Zanzibar amewaongoza Vijana kutembea Takriban kilometa 27 kwa kufanya Shughuli Mbalimbali za kijamii kwa kuyaenzi Mapinduzi ya Zanzibar.

Msafara wa Matembezi kwa Siku Ya leo Umeitimishwa katika Skuli ya Secondary Kombeni iliyopo katika Jimbo la Dimani.

Kilele Cha Matembezi ya Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar kitahitimishwa kesho siku ya Jumatatu tareh 9/1/2017 na Kupokelewa na  Mgeni RASMI  Makamo wa pili wa Rais Mhe Balozi Seif Ali Iddy pamoja na Viongozi  Mbalimbali wa chama na Serikali Katika Viwanja Vya Afisi Kuu CCM Zanzibar.
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Gadget

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu