Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
akikata Utepe kuashiria uzinduzi wa bima ya afya ya Mtoto 'Toto Kadi'
leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
amesema kuwa kiu yake katika sekta ya afya ni kuona kila mtu ana bima ya
afya.
Waziri
Ummy ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa Kadi ya Bima ya Afya kwa
Mtoto ‘Toto Kadi’ , amesema kuwa taifa kuwa lina maendeleo linatokana na
msingi wa afya ambapo msingi huo unatokana na kuwa watoto wanaopata
huduma za afya kwa uhakika.
Amesema
kuwa gharama za kulipa matibabu katika ukuaji watoto na hali uchumi
ni kubwa lakini kuwepo kwa bima hiyo kutanya wazazi kuwa na furaha
wakati wote hata ikitokea ugonjwa bima ndio inamaliza matatizo.
Ummy
amesema kuwa wakati anaingia madarakani alikutana na Rais Dk. John
Pombe Magufuli alichoendanacho ilikuwa ni kuongeza ghrarama lakini
Rais alisema hakuna kuongeza ghrama yeyote cha msingi waangalie jinsi ya
kusaidia watanzania kuwa na bima.
Aidha
Waziri Ummy amewaomba Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuja na
bima ya mama mjamzito itakayotumika wakati ujauzito na badaa ya
kujifungua.
Ummy
amesema kuwa kampeni hiyo iwe endelevu kwa nchi nzima ili watoto wote
kuwa na bima ya afya hapo tutakuwa tunajenga taifa lenye msingi bora wa
afya.Waziri
huyo ameitaka kuweka utaratibu wa kubandika mabango katika kila kumbi
za starehe ili wanavyotumia vinywaji waweze kuangalia watoto kama wana
kadi ya afya bima ya afya.
Nae
Mwenyekiti wa Bodi NHIF, Anne Makinda amesema kuwa wanafanya kazi nguvu
kuhakikisha watanzania wanapata huduma za afya pamoja na kulipa watu
wanaotoa huduma kwa bima ya afya.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
akiangalia muundo wa kadi ya bima ya afya ya Mtoto mara baada ya
kuzindua leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
akipeana Mkono na Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF, Anne Makinda mara baada
ya kuzindua bima kadi ya bima ya afya kwa watoto leo katika viwanja vya
Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF, Anne Makinda akimpa kadi Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernad Konga ,mara baaya Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy
Mwalimu kuzindua kadi ya afya ya Mtoto leo jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
akizungumza katika uzinduzi wa bima ya afya kwa mtoto katika viwanja vya
Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernad Konga akizungumza juu ya mpango wa bima
ya afya ya Mtoto katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza juu ya bima ya afya
kwa mtoto katika jiji la Dar es Salaam wakati uzinduzi wa bima hiyo
katika viwanja vya mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi
wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Dk. Dorothy Gwajima akizungumza juu ya mkakati wa wizara katika
utekelezaji wa bima ya afya.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
akipata maelezo kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernad Konga akimpa
maelezo katika banda la NHIF.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
akingalia jinsi maafisa wa NHIF wanavyofanya kazi katika usajili kadi
ya bima ya afya kwa Mtoto.
Sehemu
ya wawakilishi mbalimbali wa Sekta ya Afya na Jamii pamoja na watendaji
wa NHIF katika uzinduzi wa bima ya Afya kwa Mtoto.
Baadhi ya wananchi wa watoto wakiwa katika uzinduzi wa bima ya afya ya Mtoto katika viwanja vya Mnazi Mmoja.
Watendaji mbalimbali katika uzinduzi wa bima ya afya ya mtoto.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
akiteta jambo na Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF, Anne Makinda (Kulia) Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernad Konga.
Balozi wa Toto Kadi, Mrisho Mpoto akitumbwiza wakati wa uzinduzi wa kadi hiyo.
Mrisho Mpoto akishukuru baada ya kupewa ubalozi.
Wakicheza katika uzinduzi wa bima ambayo ni bima ya afya ya Mtoto katika viwanja vya Mnazi mmoja
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
akiwa na Watoto waliopata Kadi ya Bima ya Afya ya Mtoto.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiangalia muundo wa kdi ya bima ya afya hya mtoto.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
akimpa kadi mtoto mara baada ya kuzindua bima ya afya ya Mtoto.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja watendaji wa NHIF.
Picha mbalimbali katika uzinduzi bima ya afya ya mtoto
0 Maoni