Mkuu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa Ndugu Hassan Bomboko amekutana na kufanya maongezi na baadhi ya viongozi wa CCM na UVCCM kutoka Wilaya na Kata za Mkoa wa Dar Es Salaam.
Ndugu Bomboko ameupokea ugeni huo uliokuwa umeongozwa na Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Ilala Ndugu Hamad Pazzi, Wageni walioongozana katika msafara huo ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Temeke Ndugu Mohamed Mlingo, Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Vituka Ndugu Abubakar Jaffo na Katibu wa UVCCM Kata ya Sandali Ndugu Mrisho Kamba.
Viongozi hao kwa umoja wao wamemhakikishia ushirikiano Mkuu huyo wa Idara kwa manufaa ya UVCCM, CCM na Nchi kwa ujumla.
 |
Mkuu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa Ndugu Hassan Bomboko akimkabidhi Ngudu Mohamed Mlingo "Zungu" Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Temeke baadhi ya Majarida ya UVCCM. |
 |
Ndugu Bomboko akisalimiana na Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Ilala Ndugu Hamad Pazzi Ofisi ndogo za UVCCM Makao Makuu, Upanga Jijini Dar Es Salaam. |
 |
Ndugu Bomboko akisalimiana na Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Vituka iliyopo Wilaya ya Temeke Ndugu Abubakar Jaffo mara baada ya kumtembelea Ofisini kwake. |
 |
Ndugu Hassan Bomboko akijadiliana na jambo na Katibu wa UVCCM Kata ya Sandali, Temeke Ndugu Mrisho Kamba Ofisi kwake, Upanga Jijini Dar Es Salaam. |
0 Maoni