Unordered List


UVCCM YAMJIBU MBOWE, YAONESHA UDHAIFU WA HOJA ZAKE

Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa akisisistiza jambo mbele ya Wanahabari Ofisi ndogo za UVCCM Makao Makuu, Upanga Jijini Dar Es Salaam.








          
         VMM/U.80/8/Vol.I/73                                          20/09/2018    

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kama ambavyo Umoja wa Vijana wa CCM ulivyowaeleza hapo awali kupitia Taarifa yake  kwenu. Tunawashukuru sana kwa mwitikio wenu mzuri
1.     UVCCM inawapongeza wanachama wote wa Chama Cha Mapinduzi Nchi Nzima pamoja na viongozi wote wa CCM kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kukipigania, kukisemea na kukilinda Chama wakati wote wa kampeni,
UVCCM inawashukuru na kuwapongeza vijana wote wa Chama Cha Mapinduzi Nchi nzima kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kuinadi CCM na wagombea wake katika Uchaguzi huu mdogo. Huo ndio wajibu wetu wa msingi wa kikanuni Vijana wa Chama Cha Mapinduzi. Vijana wa CCM tuendelee kuwa imara na tuwe tayari kuitumikia Jumuiya yetu na Kukijenga Chama Cha Mapinduzi. Tunazo Chaguzi ndogo zingine katika Baadhi ya maeneo, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu 2020 hivyo Vijana tuwe tayari.
2      Umoja wa Vijana wa CCM unaipongeza Serekali ya  Awamu wa Tanokwa kazi nzuri ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2015-2020 tumeona namna ambavyo Serikali yetu katika ngazi na maeneo tofauti inavyoendelea Kuchapa Kazi na Kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
Lakini kwa kipeke Umoja wa Vijana wa CCM TAIFA unapenda kumpongeza sana  Mwenyekiti wa CCM TAIFA na Rais wa Jamhuri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi nzuri aliyoifanya katika kipindi cha miaka mitatu ya Uongozi wake. Rais Dkt John Pombe Magufuli ameweza Kumaliza mambo kadhaa wa kadhaa ambayo yalikuwa Kero na changamoto kwa Nchi yetu
Uwezo na Uweledi, Utashi wake Kisiasa,Maono na Maarifa yake makubwa aliyonayo kisiasa na kiuongozi, Dhamira na Nia ya Utumishi uliotukuka, Moyo wa kweli na wa dhati katika kuwatumikia watanzania na Tanzania kwa Uadilifu na Uzalendo mkubwa umesaidia leo hii Nchi kukimbia kwa kasi katika kujengeka kimaendeleo na kukua kwa ustawi wa jamii ya watanzania
Ndugu zangu wanahabari,
Taaluma yenu inawataka Muwe wadadisi zaidi mimi kama msemaji wa Jumuiya ya Vijana nafasi yangu inanitaka kufanya Sana Tafiti, Katika Udadisi wangu nimebaini mambo makubwa yafuatayao yaliokuwa AGENDA kubwa za Wanasiasa mwaka 2015 - 2020 na Sehemu kubwa ya Mambo hayo yalikuwa katika Ilani ya CCM leo Asilimia 70 ya Mambo hayo yametekelezeka kama ifuatavyo
1.   Kama mnavyofahamu chama chetu msingi wake ni chama cha wanyonge ndio maana ya uwepo wa jembe na nyundo
hiki kilikuwa na kitaendelea kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi. Mwl Nyerere aliwahi kusema Nchi yetu inamaadui wakubwa watatu maradhi, ujinga na rushwa. Dkt Magufuli amefanikiwa kupambana na rushwa kwa kiwango kikubwa sana mpaka sasa ndani ya miaka hii mitatu.
Katika uongozi wake aemendesha mapambano ya wazi na kupigana Vita dhidi ya adui rushwa na ufisadi Nchini. Leo hii Tanzania Imepanda kwa nafasi 13 katika Nchi zinazopigana vita ya kweli dhidi ua rushwa,ufisadi na ubadhilifu wa mali za umma katika mwaka 2016,2017 hadi sasa na imeshika nafasi ya pili kwa Nchi za Jumuiya ya Africa Mashariki katika Nchi zinazopambana na rushwa na ufisadi.
Ndugu wanahabari mtakumbuka rushwa na ufisadi ndio ilikuwa agenda namba moja ya wapinzani. Ni serikali ya awamu ya tano iliopigana vita ya vitendo kwa kuanzisha mahakama ya mafisadi na kubadilisha mifumo na muundo na viongozi wapya katika taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa, mafisadi papa wakubwa na wala rushwa wakubwa na wadogo wamepandishwa mahakamani na wengine mpaka leo hii wanasota magerezani kesi zao zikiendelea kurindima. Miaka ya nyuma ilikuwa ni mtihani mkubwa kumgusa mtuhumiwa wa uhujumu uchumi,fisadi au mla rushwa na kumpandisha kizimbani
2.     Uwajibikaji uzalendo na uadilifu kwa watumishi wa umma umeongezeka mara dufu leo Mtumishi wa Umma hana tena majivuno,kiburi wala dharau kwa wale anaowahudumia, siku hizi katika serikali ya Rais Magufuli watumishi wa Umma wana nidhamu ya kazini, weledi wenye kutumia maarifa yao kazini, Uzembe kazini sio tena agenda, wanachapa kazi wyakati zote na wanazingatia ubora na umakini kazini
3.     Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Raisi Magufuli hutumia Tsh.Bilioni 23 kutoa Elimu bure kuanzia elimu ya Msingi mpaka kidato cha nne lakini pia Serikali ya awamu ya tano imejidhatiti Kutoa Mikopo kwa wanafunzi wote wanafaulu kuingia Chuo Kikuu, haya Ni Mapinduzi makubwa katika Sekta ya Elimu
4.     Serikali ya Raisi Magufuli imefanikisha azma ya Serekali kuhamia DODOMA na Vyema tukakumbuka azma ya kuhamia Dodoma iliasisiwa na kushindwa kufanyika toka Enzi ya Utawala wa awamu ya kwanza Chini ya Rais Mwalimu Julius Kambarage Nyerere lakini ndani ya Kipindi Kifupi Cha Miaka Miwili tu Serikali ya awamu ya tano imeweza Kutekeleza azma hiyo ya Muda mrefu.
5.     ujenzi wa Miundombinu ya Kipeke na ya kisasa. kupitia Serikali ya awamu ya Tano ya Raisi Magufuli tumeshuhudia :
Flyover  Mpaka hivi ninavyozungumza na nyie tayari Serikali ya Rais magufuli imeshafungua Flyover ya Mfugale ambayo iko tayari na inatumika huku ile ya Ubungo Ikiendelea kujengwa. kwa flyovers izi mbili za Ubungo na Tazara msongamano utapungua kwa kiasi kikubwa sana
Ujenzi wa reli ya kisasa kwa kiwango cha standard gauge mpaka juzi tayari tulikuwa tumeshatandaza mataluma kwa Umbali wa kilomita 53 hapa Tunazungumiza Standard Gauge Reli inayotumia umeme na inayokwenda kwa kasi, haikuwahi kutokea Tangu Tanzania Iumbwe
Upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa mwalimi Nyerere Termina III unajengwa kwa kasi kubwa sana na Uwanja huu ukikamilika utakuwa na Hadhi ya kimataifa haswaa na umeshakamilika kwa zaid ya ssilimia 80
Mradi wa ujenzi wa Umeme wa stiglers Gorge utakao kuwa chanzo kingine cha Umeme na hivyo kumaliza kabisa  tatizo la Umeme Nchi nzima, umeme huu ambao n muhim sana kwa Viwanda tunavyoendelea kuvijenga.
Mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kule tanga mpka uganda hoima project) ni Mradi mkubwa na wenye tija kwa Taifa utatengeneza ajira nyingi na kuleta manufaa kwa watanzania wakaazi na watu wa miji ya Karibu
6.     Kufufuka kwa Mashirika ya Umma
Mashirika haya yalikuwa yameshajifia, lakin leo yamefufuliwa na yanatoa gawio kwa serikali. Mfano.

TTCL leo limefufuka na  kurejea katika hadhi na ubora wake wa utoaji wa huduma ya mawasiliano kwa njia ya simu kwa gharama nafu, tumeona katika kampeni mbalimbali na jitihada zinazofanywa na watumishia shirika hili kuendelea kulipa nguvu baada ya serikali Kununua hisa zote na
Shirika la Ndege Tanzania Moja kati ya Mambo Makubwa aliyoyafanya Rais ni upande wa ndege mpaka sasa Tanzania Tunaumiliki wa ndege Kubwa sita za kwetu pamoja na Ndege Kubwa Dreamliner ambayo imeshaanza ruti zake katika Mikoa mbalimbali
Na hivyo kuongeza pato la taifa hasa kwenye sekta ya utalii kwa kuwa hv karibun itaanza safari za kimataifa zitakazowapunguzia watalii gharama mbalimbali walizokuwa wanapitia nchi zingine kuingia tanzania.
Kuhusu madai ya CHADEMA kupitia mwenyekiti wao kuhusu uchaguzi uliofanyika juzi ambapo CCM iliibuka kidedea,
Ndugu wanahabari. Labda tu niseme kwamba, hawa ndugu zetu Chadema na madai yao ya siku zote tumekwisha yazoea kama ifuatavyo:-
1.   Wakishinda uchaguzi au kesi mahakamani dhidi ya serikali huwa wanasema *Tume ya uchaguzi au Mahakama* imetenda haki
2.   Wakishindwa huwa wanasema *Tume ya uchaguzi sio huru na Mahakama zetu sio huru*
Swali la kujiuliza ni kwamba, uhuru wa hizi taasisi zetu nyeti za nchi ni pale tu zinazowapa ushindi?
Lakin ndugu waandishi wa habari pamoja na hayo tunawajibu wa kuwajibu na kuwakumbusha mambo yafuatayo kulingana na madai ya jana.
Kwanza kabisa, ningependa mzifahamu sheria mbalimbali zinazohusu chaguzi zilizofanyika majuzi.
1.     Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977
2.     Thebpolitical parties Act
3.     Sheria ya taifa ya uchaguz suravya 343 R.e 2015
4.     The local govt elections Act cap 292 R.e 2015

Hoja zao zilikuwa ni:-
1.     Militarization of the electoral process. Polis na majeshi yanakuja  
kwenye kampen kutisha raia na bendera nyekundu kwenye magari.
Majibu. Ulinzi wa wananchi na mali zao, pia amani na utulivu n jukumu namba moja la jeshi ka polis.
Chin ya sheria ya polisi and auxiliary services Act part V
Inawataka polisi kuhakikisha kuna  utulivu wakati wa kampen.
Kwahio sio militarization bali n utekelezaji wa majukum ya polis.
2.     Sanduku la kura sio tena mwamuzi wa nan awe kiongozi_ mwamuzi n MAGUFULI tu ambae alisema "yaan nikuajiri, nikupe gari nikulipe mshahara na bado umtangaze mpinzani kashinda" kauli hio imegeuzwa sheria. Rais atambue nchi inaongozwa na Sheria na Katiba.
3.     Kukamatwa kwa mawakala wa chadema kuwekwa ndani zaidi ya masaa 24 ambapo walikuwa wakitimiza haki zao ambayo ni haki ya Chama cha Siasa kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi na kanuni zake.
4.     Wasimamizi wa uchaguzi kwa kushirikiana na CCM wanawahujumu mawakala wa Chadema kwa kuwanyima barua zao za utambulisho hivyo kuzuiwa kuingia ndani siku ya uchaguzi.
5.     Makada wa CCM, Makatibu wa CCM Mikoa, Wilaya ndio wanaopeleka majina ya nani awe msimamizi wa uchaguzi sio uchaguzi unasimamiwa na wana CCM .
6.     Polisi wanashirikishwa kuhalalisha matakwa ya CCM na ndio maana Makonda alifanya sherehe na Wakuu wa vyombo vya ulinzi.
7.     Mfumo mzma wa uchaguzi haufuati sheria, mfano.  Majina ya wasimamizi wa uchaguzi hayawekwi wazi mapema ili kuzuia objections/ pingamizi kutoka kwa Chadema kwakuwa wasimamizi wanakuwa ndio makada wa CCM anazo taarifa za ndani kutoka CCM kuhusu hilo.
8'      Kulikuwa na vituo feki vya uchaguzi 16 vyenye wapiga kura zaidi ya 7,000, wamelalamika na hawajasikilizwa
9'      Watendaji na watumishi wa serikali wanazuiliwa na sheria kujihusisha na kampeni  za uchaguzi. Lakini katika chaguzi hizi tumewashuhudia ma DC, RC na Mawaziri wakijihusisha moja kwa moja na wakitoa ahadi mbalimbali za serikali  majukwaani kwenye kampeni tena wakitumia magari ya serikali mfano Lukuvi na Makonda.
10.    Magari ya serikali wanapatiwa wagombea mfano Monduli mgombea wa CCM alipatiwa gari la serikali na Mkurugenzi.
11'    fomu za uchaguz ni tofauti na matokeo.
_ ukonga ina wapiga kura 70,000
_ waliojitokeza hawazidi 30,000
_ lakin matokeo in kura zaid ya 88,000
Maamuzi.
1'      Kutokushiriki chaguz zote zilizotangazwa na tume
2.     Kwenda Mahakamani
3.     Hoja.
Ibara ya 5 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa haki ya kupiga kura kwa kila raia wa Tanzania aliekidhi vigezo kama umri n.k kupiga kura katika uchaguzi wowote ule.
Kwa hali hii ni haki ya kila mtanzania kupiga kura na kuamua aongozwe na nani na kiongozi yupi. Kusema kuwa mwamuzi wa nani awe kiongozi na Rais pekee inakuwa sio sahihi kwa sababu Rais pekee sio mtanzania pekee alietimiza masharti bila ya kupiga kura bali ni kila mtanzania alietimiza umri wa miaka 18 na sifa zinginezo.
Ibara ya  7 ya sheria ya Taifa ya uchaguzi sura ya 343, kama ilivyorejelewa mwaka 2015 inasema Wakurugenzi wote wa Halmashauri, Miji  na Wasimamiz/ Wakurugenzi wa Uchaguzi katika Wilaya zao.  Suala la Ukada . Huenda walikuwa makada kabla ya kuchaguliwa kuwa Wakurugenzi lakini kwa sasa ni watumishi wa umma na wapo kuwatumikia wanannchi wote bila kujali chama na ndio maaana Wakurugenzi hawahawa ndio wanaopeleka miradi ya maendeleo mpaka kwa majimbo au Kata za upinzani.

Hoja ya tatu. Kukamatwa     kwa mawakala wa CHADEMA .
Katika chaguzi kuna taratibu zake ambazo wakala yeyote yule anatakiwa kuzifuata. Kama zisipofuata basi hatua stahiki zaweza kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na kukamatwa kwa muhuska.
mawakala wa CHADEMA hawako juu ya sheria kwamba kama hawajafuata utaratibu wasikamatwe.
Pia Ibara ya 86 ya sheria ya Taifa ya uchaguzi inasema kutokuwepo kwa wakala wakati wa kupiga na kuhesabu kura hakubatilishi matokeo ya uchaguzi.
Kwa hiyo wafuate sheria zote hakuna atakayewasumbua
Kuhusu hujuma kwa mawakala wa Chadema. Nimelieleza katika hoja namba tatu.
Pia sidhani kama hujuma inaweza kufanyika kwa sababu kuna kiapo wanachokula wasimamizi wa uchaguzi katika section 9(2) ya sheria ya uchaguzi 7. Mimi sio tume ya uchaguzi na siko kwa niaba yao kiongozi sisi kama chama cha siasa tuliyaona majina ya wasimamizi wa uchaguzi yalibandikwa mapema sana Mfano ukonga.
Na hiyo ni kwasababu ya matakwa ya kisheria yanayowataka tume ya uchaguzi kufanya hivyo 
12.    Kuhusu vituo feki.  Sheria inawataka tume ya uchaguzi kuvitangaza mapema vituo vyote vitakavyotumika. Kama kulikuwa na vituo feki  ilitakiwa wao wachukue hatua kwasababu vilitangazwa na kubandikwa mapema.
Ndugu wana habari, ama kweli mfa maji haaachi kutapatapa.
Hakukuwa na kituo hata kimoja kilichokuwa feki.
Asiekubali kushindwa sio mshindani
13.    Waziri na Kada wa chama chake. Endapo kuna uchaguzi na chama chake kinakuwa kinachuana.  Na anapokuwa hapo jukwaani anakuwa ni mwanachama wa kawaida wa chama husika hivyo anakuwa anafanya kazi ya chama.
Ndio maana hata mh mbowe n kiongoz wa kambi ya upinzan bunge. Na anatumia facilities zote za serikali.  Lakini katika uchaguzi anaongoza mashambulizi.
14.    Pia Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Mikoa au Mawaziri au Makatibu Wakuu wanaweza kufanya hivyo endapo kutakuwa na upotoshwaji wowote uliofanywa kwa minajiri ya kuweka sawa rekodi ya maneno ya upotoshaji. Lakini ndugu wanahabari tumesikia wametangaza kutokushiriki chaguzi. Napenda kuwaambia kwamba Kushiriki au kutokushiriki uchaguzi, nayo ni Demokrasia Katika nchi ambayo vyama vyake vya Siasa viko huru katika kushiriki au kutokushiriki uchaguzi ni ishara tosha ya ukuaji wa Demokrasia

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI


Hassan O. Bomboko
KATIBU WA IDARA YA HAMASA NA CHIPUKIZI

 






Chapisha Maoni

0 Maoni