Mtunzi: Edimund I. Lihawa,
Kidugala,
S. L. P. 999 Njombe.
0765 861 267.
Ushairi: HAPA KAZI TU! USEMI WA KISHUJAA!
1. Wangapi wamethubutu, kusema mungu asante,
Kwa mvua ya kishitu, jua lilo kali kote,
Hakunalo jema kwetu, lipi twataka tupate,
Hapa kweli kazi tu, usemi wa kishujaa.
2. Tumegeuzwa pamoja, sasa twaenda kwa kasi,
Uzalendo sasa waja, wapenda kazi si hasi,
Hatutaki tena ngoja, viwanda mwendo wa kasi,
Hapa kweli kazi tu, usemi wa kishujaa.
3. Kila jambo na nyakati, sasa tumezifikia,
Viwanda zake nyaketi, hakuna wa kupingia,
Uamuao wakati, kamwe si mpinga nia,
Hapa kweli kazi tu, usemi wa kishujaa.
4. Ni wapi tulikotoka, hatua tumezifanya,
Tumejaribu kufika, makubwa hatukufanya,
Sasa ni muda mwafaka, makubwa haya kufanya,
Hapa kweli kazi tu, usemi wa kishujaa.
5. Myaka mitatu mbioni, kwetu unathibitisha,
Hapa kazi tu ni nini, kazini twajibidisha,
Daima u kileleni, njia unatuonesha,
Hapa kweli kazi tu, usemi wa kishujaa.
6. Barabara kila pande, kamilishwa na kuanza,
Zilokuwa nazo pinde, zimekwisha nyoshwa kwanza,
Mwenge mbio kila pande, uzinduzi watufunza,
Hapa kweli kazi tu, usemi wa kishujaa.
7. Nyumba karibu wabeza, walaumu falusafa,
Hapa kazi imekaza, wenye kulimbika wafa,
Wanyonge nje ya kiza, wampa shujaa sifa,
Hapa kweli kazi tu, usemi wa kishujaa.
8. Kwa kasi sasa twaona, madeni yanapungua,
Kwaminika tunaona, twenda kujitegemea,
Mengi makubwa yafana, pasipo wategemea,
Hapa kweli kazi tu, usemi wa kishujaa.
9. Tazama kaka na dada, toka nyumba za jirani,
Kwao kwaminiwa shida, watupa shada njiani,
Huku kwa shuja si shida, wote kuja ni mbioni,
Hapa kweli kazi tu, usemi wa kishujaa.
10. Shuja wetu hana hofu, milima aparamia,
Mingi yajawa na hofu, kutumbuliwa hofia,
Kodi malipo hafifu, yashindwa myoyo tulia,
Hapa kweli kazi tu, usemi wa kishujaa.
11. Pita sasa kila kona, si nje nyumbani mwetu,
Kila monae kijana, mwendo wake kazi tu,
Shuja nguzo ya vijana, kujenga viwanda vyetu,
Hapa kweli kazi tu, usemi wa kishujaa.
12. Asante mwenyezi mungu, ahsante kwa wema wako,
Shuja umetupa mungu, kwetu furaha fuliko,
Twache fikiri kiwingu, mbali weka tarajiko,
Hapa kweli kazi tu, usemi wa kishujaa.

0 Maoni