Unordered List


MJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA KUTOKEA (M) MOROGORO NDG. REHEMA KASANGA AONGOZA HARAMBEE KATIKA SHULE YA MSINGI MISUFINI A



Mjumbe wa Baraza Kuu Uvccm Taifa Kutokea (M)Morogoro Ndugu Rehema Kasanga aongoza Hamasa na Harambee kwa ajiri ya Kufanya Ukarabati wa Baadhi ya Miundombinu ya Shule ya Msingi Misufini A ambayo Paa lake liliezuliwa na Mvua Kali.

Aidha Ndugu Rehema Kasanga  Amewaomba wananchi wote wenye Moyo wa kutoa kuweza kuisaidia Shule ya Misufini A ili iweze kukarabati miundo Mbinu yake kwa lengo la wanafunzi waweze kusomea Katika mazingira rafiki.

Mwisho Ndugu Rehema Kasanga Aliweza kufanikisha Kupatikana kwa Baadhi ya vifaa Katika harambee hiyo vikiwemo  mifuko ya saruji na Pesa Taslim.

Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM TAIFA kutokea Mkoa wa Morogoro Ndg Rehema Kasanga akihamasisha wananchi kujitoa kwa ajili ya kupigania maendeleo ya wanafunzi mashuleni kwa kuwawekea mazingira bora na rafiki kwa kusomea
Walimu na wageni waalikwa wakiwa meza kuu

Chapisha Maoni

0 Maoni