Mtunzi: PAULO NYAMOHANGA
Mbeya, Tanzania
Mawasiliano: 0758955592
Ushairi: "AMEZALIWA RAIS BINGWA JPM"
1. Leo hii kumbukizi, ya Rais kuzaliwa,
Amebariki mwenyezi, yote yameenda sawa,
Huyu mpenzi wa kazi, leo hii kazaliwa,
Pongezi kwako Rais, John Pombe Magufuli.
2. Pongezi pia natoa, kwa wote wako wazazi,
Kwa kuzaa na kulea, huyu wetu kiongozi,
Mlijenga Tanzania, kwa mtu mpenda kazi,
Pongezi kwako Rais, John Pombe Magufuli.
3. Uliyopata malezi, mema yasiyo mawaa,
Kwa wazazi na walezi, kweli walikuandaa,
Hatimaye hiyo ngazi, urais kufikia,
Pongezi kwako Rais, John Pombe Magufuli.
4. Kwenye wako uongozi, mengi umeyatatua,
Meondoa upuuzi, wa kodi kupuuzia,
Meweka wasaidizi, wilaya hata mikoa,
Pongezi kwako Rais, John Pombe Magufuli.
5. Dhuruma umeondoa, kwa wamama na vijana
Wanafunzi watambua, msaada uso hiana,
Elimu wanapokea, pasipo na kulumbana,
Pongezi kwako Rais, John Pombe Magufuli.
6. Kwa Tanzania ya kazi, mbele inaendelea,
Uliongoze jahazi, ufukweni kufikia,
Yule aso penda kazi, halali kumtumbua,
Pongezi kwako Rais, John Pombe Magufuli.
7. Maendeleo twataka, sisi sote Tanzania,
Gurudumu litafika, wanyonge wafurahia,
Furaha itawafika, matunda kujichumia,
Litadumu jina hili, Tanzania ya amani.
8. Rais upo makini, kuongoza Tanzania,
Imenenwa duniani, nchi yetu Tanzania,
Sasa wanaitamani, watamani kuhamia,
Watanzania hongera, kwa kiongozi makini.
9. Tamati nakutakia, kazi njema kiongozi,
Nchi hii Tanzania, aibariki mwenyezi,
Zanzibari bara pia, tulinde Mungu mwenyezi,
Nia ya kujivunia, Tanzania nchi ya kazi.

0 Maoni