Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison
Mwakyembe akiongea na wataalamu wa lugha ya Kiswahili ( Hawapo katika
picha), jana Jijini Dodoma katika halfa ya kuwatunuku vyeti vya
utambuzi wataalamu 67 waliofuzu mafunzo ya muda mfupi yaliyoandaliwa
na Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) jana Jijini Dodoma..
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison
Mwakyembe (Kushoto) akivishwa skafu na kijana wa Skauti wa Shule ya
Sekondari Dodoma Vicky Jactan (Kulia) , alipowasili shuleni hapo jana
Jijini Dodoma katika hafla ya kuwatunuku vyeti vya utambuzi wataalamu 67
wa lugha ya Kiswahili waliofuzu mafunzo ya muda mfupi yaliyoandaliwa
na Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA).
Mhitimu ambaye ni Mwalimu wa shule ya Sekondari Chikole ya
Jijini Dodoma Bibi. Neema Mkobalo akisoma risala kwa mgeni rasmi Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Wa
tatu kulia) katika halfa ya kuwatunuku vyeti vya utambuzi wataalamu 67
wa lugha ya Kiswahili waliofuzu mafunzo ya muda mfupi yaliyoandaliwa
na Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) jana Jijini Dodoma.
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison
Mwakyembe (Kulia) akimkabidhi cheti mmoja wa wahitimu wa mafunzo ya
muda mfupi ya wataalamu wa lugha ya Kiswahili Mwalimu wa Shule ya
Msingi Chikowa Bibi. Theresia Lejale jana Jijini Dodoma.
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison
Mwakyembe (Kulia) akimkabidhi cheti mmoja wa wahitimu wa mafunzo ya
muda mfupi ya wataalamu wa lugha ya Kiswahili Mwalimu wa wa Shule ya
Msingi Vikonje Bw. Emmanuel Mzumya jana Jijini Dodoma.
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison
Mwakyembe (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa
lugha ya Kiswahili waliofuzu mafunzo ya muda mfupi yaliyoandaliwa na
Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) jana Jijini Dodoma.(Picha na
Lorietha Laurence-WHUSM,DODOMA)
Na. Lorietha Laurence-WHUSM, Dodoma
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison
Mwakyembe amesema kuwa lugha ni kielelezo na sehemu muhimu ya
utambulisho wa taifa lolote duniani.
Hayo ameyasema jana Jijini Dodoma katika Hafla ya
kuwatunuku vyeti vya utambuzi wataalamu 67 wa lugha ya Kiswahili
waliofuzu mafunzo ya muda mfupi yaliyoandaliwa na Baraza la Kiswahili
la Taifa (BAKITA).
“Taifa lolote lisilo na utamaduni wake ni taifa mfu, na sisi
tunajivunia kwa kuwa na utamaduni hai ikiwemo lugha yetu ya Kiswahili”
alisema Dkt. Mwakyembe
Aidha aliongeza kwa kueleza kuwa lugha ya Kiswahili ni
kitambulisho cha utamaduni wa Mtanzania , kwa kuwa ndiyo lugha
inayowaunganisha watu katika shughuli mbalimbali za Kijamii, Kisiasa na
kiuchumi.
Dkt. Mwakyembe anazidi kufafanua kuwa takribani lugha elfu
sita (6000) huzungumzwa kila siku duniani ambapo lugha ya Kiswahili
ni miongoni mwa lugha 10 zinazoongelewa kwa wingi.
“Mafunzo haya ni mwanzo tu mwa mambo mengi mazuri ambayo Wizara yangu imepanga kufanikisha na ukizingatia kampeni ya mwaka huu ya Uzalendo na Utaifa ina kauli mbiu inayohamasisha kukuza lugha yetu ambayo ni Kiswahili Utashi Wetu, Uhai Wetu” alisema Dkt. Mwakyembe.
Naye Kaimu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA)
Bibi. Consolata Mushi alieleza kwamba mpaka sasa Baraza limefanikiwa
kutoa mafunzo kwa wataalamu 350 ambapo jumla ya wataalamu wapatao 198
tayari wametunukiwa vyeti na wataalamu 98 wanatarajiwa kutunukiwa vyeti
hivyo mwezi Desemba 2018.
Anazidi kueleza kuwa lengo la BAKITA ni kuwapa fursa
wataalamu hao ili waweze kusajiliwa katika mfumo wa kanzi data ambayo
tayari imesajili wataalamu wapatao 380 kwa ajili ya kufundisha lugha ya
Kiswahili kwa wageni ndani na nje ya nchi.
Pia Bibi. Consolata alitoa wito kwa wataalamu wa Kiswahili
kutoka katika mikoa yote ya Tanzania Bara kujiunga na kupata mafunzo
hayo ili waweze kuorodheshwa katika kanzi data hiyo kwa ajili ya
kukibidhaisha Kiswahili katika mataifa mengine.
Kwa niaba ya wahitimu wenzake Mwalimu wa shule ya Sekondari
Chikole ya Jijini Dodoma Bibi. Neema Mkobalo alimshukuru Waziri Dkt.
Mwakyembe pamoja na uongozi wa BAKITA kwa kuratibu mafunzo hayo na
kuahidi kufanyia kazi yale yote waliyojifunza .

0 Maoni