Unordered List


NAIBU WAZIRI WA MAJI MH. JUMAA AWESO ATIMUA MKANDARASI MRADI WA MAJI BOGA -MENGWA WILAYANI KISARAWE.

1
Naibu Waziri wa maji Mh. Jumaa Aweso akizungumza mara baada ya kukagua mradi wa Boga- Mengwa ambao umesimama baada ya mkadarasi kushindwa kuanza kazi kwa wakati kulia ni  Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mh. Jokate Mwegelo.

2
Naibu Waziri wa maji Mh. Jumaa Aweso na  Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mh. Jokate Mwegelo wakimsikiliza Mhandisi wa maji wilaya ya Kisarawe Bw. Maggid Mtili alipokuwa akieleze kadhia hiyo kwa Naibu waziri.
3 4
Mhandisi wa maji kutoka DAWASA Bw. Ishmael Kakwezi akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Maji Mh. Jumaa Aweso wakati alipokagua tanki la maji la  Mnarani mradi mkubwa wa maji wa Kibamba -Kisarawe kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mh. Jokate Mwegelo.
5
Naibu Waziri wa maji Mh. Jumaa Aweso na  Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mh. Jokate Mwegelo wakikagua ujenzi wa tanki la maji katika mradi mkubwa wa Kibamba -Kisarawe.
6
Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mh. Jokate Mwegelo  akitoa maelezo huku Naibu Waziri wa maji Mh. Jumaa Aweso  akimsikiliza kulia ni Mhandisi wa Maji Kutoka DAWASA Bw. Ishmael Kakwezi.
7
Naibu Waziri wa maji Mh. Jumaa Aweso  na Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mh. Jokate Mwegelo wakimsikiliza Mhandisi wa Maji wilaya ya Kisarawe Bw. Maggid Mtili alipokuwa akisoma ripoti ya mradi wa maji wa Chole- Kwara.
8
Chanzo cha maji Chole ambako limejengwa tuta kubwa.
9
Naibu Waziri wa maji Mh. Jumaa Aweso  na Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mh. Jokate Mwegelo wakikagua tuta la chanzo cha maji Chole-Kwala
………………………………………………………………………


Naibu Waziri wa maji Mh. Jumaa Aweso ameifukuza Kampuni ya Mazongela Building   iliyopewa kazi ya kujenga mradi wa maji wa Boga -Mengwa wilayani Kisarawe wenye thamani ya shilingi Milioni 536, kutokana na kushindwa kuanza kazi kwa zaidi ya miezi mitano toka ilipopewa kandarasi hiyo.
Mh. Jumaa Aweso akizungumza mara baada ya kukagua mradi huo  wakati alipofanya ziara katika miradi mbalimbali ya maji inayotekelezwa wilayani humo,  amesema serikali ya awamu ya tano imeweka malengo makubwa ya utekelezaji wa miradi ya maji nchini.
Lakini tatizo kubwa katika maeneo mengi limekuwa ni wakandarasi kushindwa kutekeleza miradi hiyo kwa wakati na wengine kushindwa kabisa kuanza kazi yenyewe.
Mh. Aweso ameziasa halmashauri mbalimbali nchini kuhakikisha wanawapa kazi wakandarasi wenye uwezo wa kufanya kazi na siyo wababaishaji kama ilivyotokea kwa kampuni ya Mazongela Building Company ambapo ameagiza kampuni hiyo isipewe kazi nyingine katika halmashauri ya Kisarawe.
Awali Mhandisi wa maji katika Halmashauri hiyo Bw. Maggid Mtili alimueleza Naibu Waziri kuwa amejaribu mara kadhaa kumuandikia barua mkurugenzi wa kampuni hiyo Bw. Salum Suleiman Ally, lakini amekuwa akikaidi na hajawahi kufika ili kuanza kutekeleza  mradi huu.
“Mh. Waziri hata katika ziara hii alitakiwa kuja kwa sababu tulimuandikia barua tukamtaarifu kuhusu ujio wako lakini kama unavyoona haonekani kwenye ziara”. Amesema Mhandisi huyo.
Naye Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mh. Jokate Mwegelo akizungumza katika ziara hiyo amesema “Tatizo kubwa kwa wananchi wa  Kisarawe ni maji,  na Mh, Rais Dk. John Pombe Magufuli amefanya kazi kubwa ambapo Tangu uhuru awamu hii ya tano Kisarawe kunatekelezwa miradi mikubwa sana ya maji”.
Amemshukuru Mh. Rais John Magufuli  kwa moyo wake wa kizalendo kwa wanakisarawe na kuwasihi watendaji wote wilayani humo kumuunga mkono Mh. Rais na kuhakikisha wanasimamia utekelezaji wa miradi hiyo kwa nguvu zote ili ikamilike na kuondoa tatizo la maji wilayani humo.

Chapisha Maoni

0 Maoni