USHAIRI: HONGERA BABA DKT. BASHIRU (MWAKA MMOJA WA UKATIBU MKUU CCM) Mtunzi: Edimund Lihawa S.L.P 999 Kidugala, NJOMBE Simu no; 0765861267 1. Daktari wetu Bashiru, we u jiwe la msingi, We hukuja kwa udhuru, lako moja siyo mengi, Haki amani Bashiru, wasisitiza kwa wingi, Hongera baba bashiru, mwaka sasa umefunga. 2. Ishina9 mei mwezi, shirini kumi na nane, Ulipata uteuzi, chama na kionekane, Kweli umepiga mbizi, chama sasa ni kinene, Hongera baba bashiru, mwaka sasa umefunga. 3. Umepambana vikali, juu ya makinikia, Umefunua ukweli, sisi tunajivunia, Twanufaika twakili, kwa uchumi Tanzania, Hongera baba bashiru, mwaka sasa umefunga. 4. Na ndani ya chama chetu, ni Chama Cha Mapinduzi, Udugu hata na utu, na umoja si upuzi, Na wakumbatia vitu, wametoka kama wezi, Hongera baba bashiru, mwaka sasa umefunga. 5. Umepandisha uchumi, wa Chama Cha Mapindui, Vyanzo vingi vya uchumi, nondo hawaingilii, Falsafa za uchumi, ni nyingi yako ni hai, Hongera baba bashiru, mwaka sasa umefunga. 6. Usimamizi wa dhati, kutekeleza wajibu, Kweli li wazi kwa dhati, matendo mengi yajibu, Chamani watii kwa dhati, hakuna shughuli bubu, Hongera baba bashiru, mwaka sasa umefunga. 7. Ona ye alivyo bingwa, kwenye mambo ya uchumi, Kadi za umeme undwa, vyote vyanzo vya uchumi, Ufujaji kuondoshwa, chama chalinda uchumi, Hongera baba bashiru, mwaka sasa umefunga. 8. Vijana hujawaacha, kweli we ni dila kwao, Wao ni kila kukicha, wewe ni kioo kwao Ujamaa hatutaacha, kutoka kwako tunao Hongera baba bashiru, mwaka sasa umefunga. 9. Tokeo la chama chetu, taifa lajivunia, Kukua kwa chama chetu, ni taifa linakua, Hongera Bashiru wetu, twafurahi Tanzania, Hongera baba bashiru, mwaka sasa umefunga. 10. Twakuombea kwa mungu, we kiongozi shupavu, Wazi kakuleta mungu, nchini tingisha nyavu, Haya si maneno yangu, watanzani kwa nguvu, Hongera baba bashiru, mwaka sasa umefunga. 11. Pagam Amum mwalim, chuo kiku UDSM, PS 2 mwalim2, 21 ni mwalim, Kafananisha mwalim, na viongozi muhim, Hongera baba bashiru, mwaka sasa umefunga. 12. Karamu napumzisha, uwe na sherehe njema, Katika huu mwaka kwisha, fanya tafakari njema, Hakuna tanga kushusha, sisi daima tu nyuma, Hongera baba bashiru, mwaka sasa umefunga.
0 Maoni