Unordered List


MABALOZI WA TANZANIA NA NJE YA NCHI WAFANYA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO ZANZIBAR

Na Thabit Madai, Zanzibar.
Zaidi ya Mabalozi 32 wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi wamefanya ziara visiwani Zanzibar ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ)  na  ile miradi ya wawekezaji binafsi.

Katika ziara hiyo mabalozi hao walipata fursa ya kutembelea Ujenzi wa maduka ya biashara (Shopping mall) Michenzani, Ujenzi wa jengo la Abiria terminal III  katika kiwanja cha Ndege cha kimatiaifa cha Sheikh Abeid Amani karume, Mnara wa Kumbukumbu ya Hayati Sheikh Abeid Amani Karume na  Ujenzi wa Nyumba za kisasa Fumba.
Maeneo mengine Mabalozi hao walitembelea ni ujenzi wa barabara na Daraja pamoja na ujenzi wa eneo maalum litakalo tumika kuhifadhia mafuta eneo la Mangapwani kaskazini Unguja.

Chapisha Maoni

0 Maoni