Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM Tanzania Bara Ndugu Galila Wabanh'u (MNEC) akizungumza na Vijana Watafsiri Movie za Nje katika Ofisi ndogo za Makao Makuu ya UVCCM Taifa jijini Dar es salaam. ............................................
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM Tanzania Bara Ndugu Galila Ramadhan Wabanh'u (MNEC) amekutana na kufanya mazungumzo na Wasanii wa Kutafsiri kwa Lugha ya Kiswahili katika Movie za nje kutoka Wilaya ya Temeke jijini Dar es saalam.
Katika Mazungumzo hayo Umoja wa Watafsiri Movie za Nje kwa Lugha ya Kiswahili walifikisha Changamoto zao kwa Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa-Bara Ndugu Galila (MNEC) na kuomba zitendewe haki kwakuwa Chama cha Mapinduzi kinashughulika na shida za watu mbalimbali.
Naibu Katibu Ndugu Galila Wabanh’u alipokea Changamoto za Watafsiri Movie za Nje na kuwapongeza kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kukuza Lugha ya Kiswahili.
Pia, Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Bara aliomba kushughulika na Changamoto hizo ndani ya wiki moja ili kupata ufumbuzi wa suala la kurasmishwa na serikali Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aidha, Naibu katibu Mkuu wa UVCCM Bara amepokea mchango wa Umoja wa Watafsiri Movie kwa lugha ya Kiswahili Tanzania unaoenda kwa wahanga wa Ajari ya Moto iliyotokea hivi karibuni Mkoa wa Morogoro na kuahidi kufikisha kwa walengwa.
|
0 Maoni