Kamati ya utekelezaji ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Iringa imeendelea kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo yakiwa ni matokeo ya utekelezaji yakinifu wa ilani ya uchaguzi ya CCM katika nchi yetu. Kamati hiyo chini ya kiongozi wake comrade Kenani Labani Kihongosi leo ilitia nanga katika wilaya ya Iringa mjini.

Kamati ya utekelezaji ya UVCCM mkoa wa Iringa leo imetembelea miradi mikubwa mitatu ya maendeleo ambayo kimsingi inaendelea kujengwa na mingine ikiwa imekamilika kabisa na kufanya kuwa kivutio kikubwa mno kwa wananchi wa wilaya ya Iringa DC na mkoa wa Iringa kwa ujumla kwa jinsi ilivyochangia kutatua kero kubwa zilizokuwa zinaikabili wilaya hiyo.
Kamati ya utekelezaji UVCCM mkoa wa Iringa imepata kutembelea *Hospitali mpya kabisa ya wilaya ya Iringa iliyojengwa katika taarafa ya Pawaga. Hospitali hiyo ambayo ni miongoni mwa hospitali 70 za wilaya zilizojengwa nchi nzima kwa fedha zilizo tolewa na Mh Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli* aliahidi na ametekeleza kuhakikisha anaboresha sekta ya afya ndani ya mkoa wetu na nchi nzima kwa ujumla. Hospitali hiyo iliyogharimu kiasi cha TZS 1.5 billion mpaka sasa imekamilika kwa asilimia 100 na baadhi ya madaktari watatu (3) tayari wameshafika, hivyo hospitali hiyo inahitaji kuletewa dawa ili ianze kutoa huduma za afya ambazo imeonekana kuwa tatizo kubwa kwa wakazi wa wilaya na tarafa hiyo ya Pawaga.
Sambamba na hayo, kamati hiyo ya utekelezaji ya UVCCM mkoa wa Iringa ilitembelea Mradi mkubwa wa ujenzi wa Chuo Cha VETA unaondelea ndani ya wilaya hiyo. Chuo hicho ambacho ni agizo alilolitoa Mh Rais Dkt John Magufuli kwamba kila wilaya nchini iwe na chuo cha mafunzo stadi (VETA) ambapo kiasi cha zaidi ya TZS billion 1.5 zimetengwa kwa ajiri ya kukamilisha ujenzi huo ambao mpaka sasa msingi umeshachimbwa na ujenzi unaendelea na unatarajiwa kukamilika ndani ya muda fupi ndani ya mwaka huu wa 2020

Vilevile kiongozi huyo wa UVCCM mkoa wa Iringa alifika katika mradi mkubwa wa umwagiliaji uliopo katika tarafa hiyo ya Pawaga ambayo ni maarufu sana kwa kilimo cha Mpunga, Sikmu hiyo ya umwagiliaji inauwezo mkubwa wa kuhudumia zaidi ya hekta 1,300.
Lakini mradi huu ambao ulikuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa Iringa DC umekumbwa na dhoruba kubwa ya mafuriko yaliyotokea katika musimu huu wa mvua za masika ambao mpaka sasa miundombinu yake inahitaji gharama za sh. milioni mia nane thelathini na mbili ambapo wakulima hao wanahitaji msaada kutoka kwa wadau mbalimbali na serikalini ili kuweza kuboresha miundombinu ya skimu hiyo ili iendelee na utoaji wa huduma ya kilimo cha umwagiliaji hapo tarafani Pawaga.
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Iringa Ndugu Kenani Kihongosi alikutana na kuzungumza na Baraza Maalum la vijana Ilolo Mpya na kuwasisitiza waende kufafanua mambo mbalimbali yanayofanywa na serikali kwa wananchi. Pia katika kikao hicho maalumu wananchi walipata nafasi ya kutoa kero zao ambazo zingine zilitolewa ufafanuzi na wataalamu waliokuwepo kwenye ziara hiyo na kero zingine zilichukuliwa kama changamoto kwa ajili ya hatua zingine zaidi za utatuzi wa kero hizo.
Mwenyekiti ametoa pongezi nyingi kwa uongozi mzima wa CCM wilaya ya Iringa unaoongozwa na mwenyekiti wake ndugu Constantino Kihwele na katibu wake Mobutu Malima kwa niaba ya kamati ya siasa kwa jinsi wanavyoisimamia serikali katika kutekeleza ilani ya uchaguzi wilayani hapo. Pia mwenyekiti UVCCM mkoa wa Iringa ametoa pongezi nyingi kwa jumuiya ya umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi wilaya Iringa unaongozwa na mwenyekiti wake comrade Mapesa Juma Jonson Makala sambamba na katibu wake comrade Julius Simalenga kwa jinsi ambavyo wanashirikiana na Chama Cha Mapinduzi wilayani hapo katika kusimamia utekelezaji wa ilani ya CCM ndani ya Iringa DC.
Vilevile ndugu Kenani Kihongosi ametoa pongezi zake za dhati kwa mkuu wa wilaya hiyo Bi Richard Atufigwege Kasesela Kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya katika wilaya ya Iringa hasa katika kusimamia Miradi ya MAENDELEO kwa uaminifu na uadilifu mkubwa pia amempongeza mkurugenzi wake Robert Masunya kwa jinsi wanavyojitahidi kusimamia Miradi hiyo na kusema kuwa viongozi hao wa serikali wamekua mfano bora kwasababu ya kufanikisha miradi mikubwa ambayo kwa asilimia kubwa imekamilika ndani ya wilaya hiyo.
Pia mwenyekiti huyo alimpongeza mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh William Vangimembe Lukuvi kwa kazi nzuri na kubwa aliyoifanya na anayoendelea kuifanya katika taifa letu, jimbo la Ismani na tarafa zake zote maana katika utekelezaji wa miradi hiyo naye anamchango mkubwa wa kuisemea serikalini na sasa imetekelezwa.
Mwenyekiti wa Mkoa wa Iringa UVCCM amesema Mheshimiwa Waziri Lukuvi anastahili heshima kwa kuwakilisha wananchi wa Isimani Vizuri pia kwa kazi nzuri anayoifanya wanaisimani hawapaswi kufanya makosa katika Uchaguzi mkuu kwa kuchagua Viongozi wa Upinzani,Kazi ya Mbunge wa isimani Inajieleza na wanapaswa Kumuunga mkono.
Imetolewa na;
Isaak Almas Mgovano
Katibu Hamasa na Chipukizi UVCCM mkoa wa Iringa
0 Maoni