Unordered List


CCM YAJIFUNGIA SIKU TATU KUWAPIGA MSASA WATENDAJI WAKE JIJINI DODOMA.


Chama Cha Mapinduzi leo Jumatano 3 Novemba,2021  Kimefungua mafunzo maalum ya watendaji wa Chama ambao ni Makatibu wa Mikoa na Wilaya zote nchini.


Mafunzo hayo yamefunguliwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Ndugu Philip Japhet Mangula katika ukumbi wa NEC makao makuu ya CCM jijini Dodoma.

Pamoja na Mambo mengine ya msingi  lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo washiriki ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi na ufanisi ikiwa ni pamoja na usimamizi wa katiba, kanuni na ilani ya Uchaguzi ya CCM, maelekezo ya vikao sanjari na masuala mbalimbali ya ujenzi wa Taifa letu.

Mafunzo hayo yatafanyika kwa siku sita na zaidi ya mada 17 zitafundishwa na wakufunzi mbalimbali  waandamizi wa Chama na Serikali. 

Mafunzo hayo yatahitimishwa tarehe 6 Novemba,2021 ambapo Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufunga Mafunzo Hayo.





Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ndg Philip Japhet Mangula akizungumza wakati akifungua Semina ya Mafunzo kwa makatibu wa Chama Cha Mapinduzi Mikoa na Wilaya zote Nchini katika Ukumbi wa Halmashauri Kuu Dodoma (White House)
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Daniel Chongolo akizungumza katika Semina ya Mafunzo kwa makatibu wa Chama Cha Mapinduzi Mikoa na Wilaya zote Nchini katika Ukumbi wa Halmashauri Kuu Dodoma (White House)
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (Bara) Ndg Christina Mdeme akizungumza katika Semina ya Mafunzo kwa makatibu wa Chama Cha Mapinduzi Mikoa na Wilaya zote Nchini katika Ukumbi wa Halmashauri Kuu Dodoma (White House)
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Daniel Chongolo akiteta Jambo na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Philip Japhet Magula
Sehemu ya Wakufunzi na Washiriki wa  Semina ya Mafunzo kwa makatibu wa Chama Cha Mapinduzi Mikoa na Wilaya zote Nchini katika Ukumbi wa Halmashauri Kuu Dodoma (White House)

Wajumbe wa Sekretariet ya Chama Cha Mapinduzi Taifa 
Sehemu ya Washiriki wa Semina hiyo Makatibu wa Wilaya na Mikoa wa CCM wakinyanyua mkono wakati wa Kula kiapo Cha Mwanachama wa CCM kabla ya Kuanza kwa Mafunzo hayo,Leo Novemba 03,2021 Jijini Dodoma.
Sehemu ya Washiriki wa Semina hiyo Makatibu wa Wilaya na Mikoa wa CCM
Sehemu ya Sekretariet Ya CCM (katikati) Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM Ndg Kenani kihongosi akiimba nyimbo ya chama pamoja na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Ndg Kailima
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (Zanzibar) Dkt Abdallah Sadala Mabodi akizungumza katika Semina ya Mafunzo kwa makatibu wa Chama Cha Mapinduzi Mikoa na Wilaya zote Nchini katika Ukumbi wa Halmashauri Kuu Dodoma (White House)

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Daniel Chongolo akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg Christina Mdeme wakati wa Semina ya Mafunzo kwa makatibu wa Chama Cha Mapinduzi Mikoa na Wilaya zote Nchini katika Ukumbi wa Halmashauri Kuu Dodoma (White House). (PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI /CCM MAKAO MAKUU)


 

Chapisha Maoni

0 Maoni