Unordered List


ZIARA YA KINANA TEMEKE, AKUTANA NA VIKUNDI VYA VICOBA VILIVYOASISIWA NA MTEMVU



 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Kigamboni Dk. Faustine Ndungulile, alipowasili kwenye Ofisi ya CCM wilaya ya Temeke kwa ajili ya kuanza ziara katika wilaya hiyo leo ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya siku nne mkoani Dar es Salaam. Wapili ni Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu.
 Kinana akivishwa skavu baada ya kuwasili Ofisi ya CCM Temeke
 Kinana akitoka katika ofisi ya CCM wilaya ya Temeke baada ya kuzungumza na Kamati ya Siasa ya Wilaya hiyo, Wapili ni Mtemvu na kulia ni Mkt CCM Dsm, Ramadhani Madabida
 Kinana na Madabida wakiwa katika bajaji ya mwanachama wa VICOBA wakati Kinana, alipokuwa akienda kwenye mkutano wake na Vicoba Temeke katika ukumbi wa Kata ya 15 Pub, Temeke
 Mtemvu katika bajaji wakati wa kwenda kwenye kikao hicho na Vicoba wa Temeke
 Kinana akishuka katika bajaji baada ya kufika kwenye ukumbi wa Kata ya 15 Pub, kwenye mkutano na Vicoba Temeke. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam. Ramadhani Maadabiba.
 Kinana akiingia ukumbini na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Temeke Yahya Sikunjema kwa ajili ya kuzungumza na Vicoba wa Temeke
 Vicoba wakimshangilia Kinana alipozungumza nao katika ukumbi wa Kata ya 15 Pub, Temeke
 Msanii wa Machozi Theatre Group, akionyesha machejo Kinana alipokutana na Vicoba, Temeke
 Mtemvu akimtuza msanii wa kikundi cha Machozi Theatre Group kikundi hicho kilipotumbuiza wakati Kinana kizungumza na Vicoba wa Temeke katika ukumbi wa Kata ya 15 Pub.
 Maliki Ndembo (65) akisoma gazeti la  Uhuru nje ya ukumbi wa Kata ya 15, Temeka
 Kinana akikagua mitambo ya mradi uliokuwa wa kusafisha gesi kutoka kwenye taka eneo la Mtoni, Temeke. Mradi wenye mitambo hiyo uliopo chini ya Jiji la Dar es Salaam, haukuwahi kufanya kazi hadi sasa na sasa Halmashauri ya wilaya ya Temeke inataka uwe chini ya miliki yake ili iweze kuundeleza.
Kinana akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick baada ya kukagua eneo la mradi huo. Picha zote na Bashir Nkoromo wa CCM Blog

Chapisha Maoni

0 Maoni