Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa Ndg Kheri D. James (MCC) amewasili leo tarehe 01/10/2018 Mkoa wa Tabora tayari kwa ziara yake ya siku saba.
Ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kikazi ambapo Mwenyekiti atakagua Uhai wa Jumiya na Chama, Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015-2020 hasa kwa maswala yawa husuyo vijana.
Mwenyekiti UVCCM Taifa Ndg Kheri James akisaini kitabu cha wageni kwa staili ya aina yake ili kuwahi "Site"
Mwenyekiti Kheri James akitembelea kiwanda kinachotengeneza chaki zisizo na vumbi cha Tanza Chalks.
Kiwanda kidogo! Mwenyekiti Kheri James akisikiliza kwa makini jinsi uendeshwaji wa shughuli za kiwanda hiki kidogo
"Kazi yetu kuu ni kukijenga Chama na kushughulika na kero za wananchi hasa wanyonge"
"Tukutane Kazini"

0 Maoni