Unordered List


DC MHANDISI ZEPHANIA CHAULA AWEKA BAYANA  VIPAUMBELE VYA SIMANJIRO.



Na Maiko Luoga 

Katika Kutekeleza Ilani ya Uchaguzi  ya Chama cha Mapinduzi CCM 2015 Hadi 2020 Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara Imejiwekea Mikakati Maalumu ya Maendeleo katika Wilaya hiyo Ikiwemo Kutenga Vipaumbele vya Elimu, Afya, Maji safi na Salama Pamoja na Sekta ya Viwanda na Uwekezaji. 

Akizungumza na Mwandishi wetu kwa njia ya Simu Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara Mhandisi (Engineer) Zephania Chaula Alisema kuwa Licha ya Kushughulika na Maendeleo mengine katika Wilaya hiyo Uongozi Uliamua Kuweka vipaumbele Hivyo ambavyo Vinagusa maisha ya Mwananchi moja kwa moja Ili Kufikia 2020 Vipaumbele hivyo Viwe Vimetekelezwa kwa Asilimia Kubwa zaidi. 

Mhandisi Chaula Alisema Kuwa Vipaumbele hivyo vimeendelea Kutekelezwa Kulingana na Mahitaji ya Sekta husika kwakushirikiana na Wananchi Wa Simanjiro ambao wengi wao Aliwataja kuwa ni wafugaji wa Kabila la Wamasai Ambao Amewapongeza kwakushiriki Kikamilifu Shughuli mbalimbali Katika Wilaya yake Ambayo ni Miongoni mwa wilaya Kubwa Nchini. 

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya ya Simanjiro Alijikita zaidi katika Kuelezea Maendeleo ya Sekta ya Elimu katika Wilaya hiyo Kwakusema kuwa Alifika na Kuanza kazi katika wilaya hiyo Tangu mwaka 2016 Baada ya Kuteuliwa Na Mh, Rais Dkt. John Magufuli Kushika nafasi hiyo Akiikuta Wilaya hiyo ipo katika nafasi ya Mwisho yaani nafasi ya Saba kati ya Halmashauri Saba za mkoa wa Manyara katika matokeo ya Elimu ya Msingi ikiwa na Asilimia 49 za Ufaulu. 

"Asante sana Ndg Mwandishi kwakunitafuta na kuzungumza nami katika kipindi hiki cha Mwisho wa mwaka 2018, Leo naomba Nijikite zaidi katika Sekta ya Elimu katika wilaya hii ya Simanjiro, kwakweli nilifika Hapa tangu mwaka 2016 Nilipoteuliwa na Mh. Rais Nilikuta Wilaya ipo katika hali mbaya kielimu Ikiwa na Asilimia 49, Ndipo Nikaanza Kuchukua Hatua hatimae mwaka huu 2018 Wilaya imepanda hadi Asilimia 69 ya Ufaulu hii ni katika Elimu ya Msingi." Alisema Mhandisi Chaula. 

Aliongeza Kuwa kwasasa Ufaulu katika Wilaya yake Umepanda kutoka Asilimia 49 mwaka 2016 hadi Asilimia 69 za Ufaulu katika Elimu ya Msingi Mwaka 2018 na kuifanya Wilaya hiyo Kushika nafasi ya Tano kati ya Halmashauri Saba za Mkoa wa Manyara Huku akiweka Bayana Mbinu zilizotumika kubadili Matokeo hayo kwa kipindi cha Muda mfupi kuwa Kufanya vikao vya mara kwa Mara na Waratibu wa elimu kata, Walimu wakuu pamoja na Kukutana na Walimu na Kusikiliza Kero zao pamoja na Kuzitatua kwa wakati. 

"Lengo letu nikufikia Asilimia 80 ya Ufaulu Ifikapo mwakani 2019 Ili tuweze Kuwa katika Nafasi nzuri zaidi maana Wilaya hii kuna wakati huko nyuma ilishawahi kushika hadi nafasi ya kwanza sasa mpango wetu nikurudi katika hizo nafasi za Juu kwenye mkoa wetu, Ili kufikia Asilimia hiyo 80 Ndio tumeendelea na Mikakati ikiwa kuboresha Miundombinu mbalimbali katika Shule zetu kujenga madarasa ya Kutosha pamoja na Nyumba za walimu, pia Tumekuwa Tukitoa Motisha kwa Walimu na Wanafunzi wanaofanya Vizuri katika shule zao ili kuongeza kasi ya Ushindani". Alifafanua hivyo DC Chaula. 

Mhandisi, Zephania Chaula ni Miongoni mwa Viongozi wachache Ambao wameteuliwa na Rais Magufuli Kutoka wilayani Ludewa katika Mkoa wa Njombe Alipoulizwa Kuwa Anaitazamaje wilaya ya Ludewa Kimaendeleo ambayo Ndio nyumbani kwake Kiongozi huyo Alisema kuwa hana Shaka na Maendeleo ya Ludewa kwakuwa Mkuu wa Wilaya anayeiongoza Wilaya hiyo Mh. Andrea Tsere Ni Mchapakazi na Amekuwa akiwasiliana nae kila wakati.

Zephania Chaula Amewahi Kuwania nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Ludewa kwa Vipindi Vinne Mfululizo lakini Kura hazikutosha Hivyo ameendelea Kuwashukuru wananchi wa Ludewa waliomwamini Huku akiwataka Kuendelea Kutoa Ushirikiano kwa Viongozi walioko Madarakani pamoja na Kumshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwakumteua Kushika nafasi hiyo katika Wilaya ya Simanjiro.

"Nimeona pia Mh. Tsere Amewaalika wadau wa Maendeleo ya Ludewa katika Mkutano wa Elimu hapo February 20 Mwakani Nampongeza sana Hilo ni jambo jema namimi nitakuja Kushiriki pamoja na Kutoa Maoni yangu ili Tuweze kuboresha na Wilaya yetu, Unajua sisi Viongozi Tunapokuwa na Ushirikiano na wadau wa maendeleo pamoja na Wananchi wetu Nirahisi kupeleka Mbele maendeleo ya Taifa letu". Zephania Chaula DC simanjiro.

Chapisha Maoni

0 Maoni