Umoja wa Vijana wa CCM mkoa wa Songwe, umeendelea na Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM husasan katika Kupambana na Umaskini na Ajira kwa Vijana kwa kuanzisha mafunzo ya Ujasiriamali kwa vitendo kwa wilaya zote ndani ya mkoa kwa vijana wote na wananchi wote bila kujali itikadi za vyama vyao.
M/kiti UVCCM Mkoa wa Songwe Ndugu Andrew Kadege alisema "Kupitia ziara tuliyofanya na kamati yangu ya Utekelezaji kwa wilaya zote ndani ya mkoa wetu pamoja na changamoto nyingi tulizoziona na kukutana nazo mojawapo ilikuwa ni kutokuwa na hamasa na uelewa wa mikopo isiyo na ratiba inayotolewa na halmashauri zetu kwa makundi maalum ambapo kila halmashauri inapaswa kutenga 10% ya mapato yake ya ndani ambapo 4% ni kwa ajili ya vijana.
Mh mkuu wa mkoa kwa kuthibitisha hili Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya mji wa Tunduma katika taarifa yake ameonesha katika mwaka wa fedha 2017/18 walitenga zaidi milion 374 lakini walitoa tzs mil 100 na 2018/19 robo ya kwanza wametoa mil 70 tu hadi novemba ,hivyo tukaona ni fursa na kuamua kuwahamasisha vijana wote ndani ya mkoa wa Songwe kwa kufanya mafunzo haya ya Ujasiriamali kwa vitendo na kuwaelekeza taratibu na namna ya kuweza kunufaika na mikopo hii"
Tumetoa mafunzo mbalimbali kwa vitendo kama utengenezaji wa sabuni, dawa za kusafisha vyoo, utengenezaji batiki, tunaziomba halmashauri zote ambapo tutafikisha mafunzo haya, vikundi vitakavyokuwa vinafanya uzalishaji wa batiki basi kuelekea sherehe za uwashwaji mwenge wa uhuru kitaifa zitakazofanyika kitaifa mkoani kwetu mwakani vipewe fursa ya kufanya kazi kwa kubuni vazi la mwenge wa uhuru na hii ndio tafsiri halisi ya kuwainua vijana kiuchumi na kuelekea uchumi wa viwanda.
Mafunzo ya siku mbili yamehitimishwa leo na taasisi ya TAEDO katika halmashauri ya mji wa Tunduma ambapo yataendelea wilaya ya Ileje, Songwe,Mbozi na kumalizia halmashauri ya wilaya ya Momba.
#TukutaneKazini
#HapaKaziTu
Viongozi wa CCM na Jumuiya zake wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya mafunzo ya ujasiriamali yanayotolewa kwa vitendo na Taasisi ya TAEDO chini ya Mkurugenzi wake Ndg Kenani Kihongosi
Baadhi ya bidhaa zilizotengenezwa kwenye mafunzo hayo na Vijana waliokwisha patiwa darasa la namna ya kutengeneza batiki


0 Maoni