Manchester United wamekubali kumuuza kiungo wao wa kati, mbelgiji Marouane Fellaini, 31, kwa kima cha euro milioni 15 mwezi huu.
Tayari vilabu vya AC Milan, Porto na Guangzhou Evergrande ya Uchina vimeonesha nia ya kutaka kumsajili. (Mirror)
Chelsea
wanatarajiwa kuendelea mbeli na mpango wao wa kumsajili mshambuliaji wa
Juventus Gonzalo Higuain, ambaye yuko kwa mkopo AC Milan, kufikia
mwisho wa wiki hii. (Telegraph)
Meneja wa AC Milan Gennaro Gattuso amesema kuwa Higuain hajamwambia kuwa anataka kuondoka klabu hiyo. (Evening Standard)
Christian
Eriksen, 26,huenda akatia saini mkataba mpya na Tottenham, wakati
ambapo Real Madrid pia inapigiwa upatu kumsajili kiungo huyo wa kati
raia wa Denmark. (AS)
Arsenal wanataka winga wa Ubelgiji Yannick
Carrasco, 25, kujiunga nao lakini hawana uwezo wa kumsaini kiungo huyo
kutoka klabu ya Dalian Yifang ya Uchina.
Gunners wanaweza kufanya hivyo endapo watamuuza kiungo wao wa kati Mesut Ozil. (Fox Sports Asia)
Arsenal
watalazimika kupunguza malipo ya Ozil ya euro 350,000 kwa wiki
kumuachia nyota huyo huku kukiwa na uwezekano wake kujiunga na Inter
Milan kwa mkopo. (Mirror)
Barcelona
wanapania kumsaini mshambuliaji mpya na kuna tetesi kuwa huenda
wamnunua Cristhian Stuani, 32, wa Girona huku wakiwalenga washambuliaji
wengine kama Fernando Llorente, 33, wa Tottenham na Olivier Giroud, 32,
na Alvaro Morata, 26, kutoka Chelsea. (Marca)
Azma ya mshambuliaji
wa Chelsea Alvaro Morata ya kutaka kuhamia Atletico Madrid huenda
ikafifia kwa sababu klabu hiyo ya Uhispania inataka kumsajili Morata kwa
mkopo hadi mwisho wa msimu huu. (Mail)
Leicester huenda wanamuajiri meneja wa Celtic Brendan Rodgers kuchukua nafasi ya meneja wao wa sasa Claude Puel. (Sun)
West
Ham wamekataa ofa ya euro milioni 8.9 kutoka kwa Fiorentina ya kutaka
kumnunua kiungo wa kati wa Equatorial Guinea Pedro Obiang. (Sky Sports)
Arsenal
wanamfuatilia kwa makini kiungo wa kati wa Colombia James Rodriguez na
huenda wakalipa euro milioni 3 kwa Real Madrid ili kubadilisha miezi
sita ya mwisho ya mkataba wake wa kuichezea kwa mkopo Bayern Munich kwa
miaka miwili.(Mail)
Bournemouth
wanatarajiwa kuweka dau la euro milioni 15 kumnunua beki wa kati wa
Brentford na Wales Chris Mepham, 21, ili kumzuia asijiunge na
Southampton. (Sun)
Chelsea wameongeza ofa ya euro milioni 36
kumnunua kiungo wa kati wa Argentina Leandro Paredes, 24, kutoka Zenit
St Petersburg ya Urusi.(Star)
Mshambuliaji wa West Ham na Mexico
Javier Hernandez, 30, anataka kujiunga na Valencia, lakini Hammers
huenda wasimuachilie hadi wapate mchezaji atakayechukua nafasi yake.
(Guardian)
Manchester United wameanza mazungumzo na Tromso kumhusu
Isak Hansen-Aaroen ili kuzima azma ya Everton na Liverpool kumnunua.
(Aftenposten, via Manchester Evening News)
Manchester City hawana mpango wa mpango wa kumnunua Isco ambaye ni kiungo wa kati wa Real Madrid na Uhispania. (ESPN)
Kipa
wa Real Madrid Kiko Casilla, 32, alikosa kufika mazoezini siku ya Juma
nne na badala yake kusafiri England kufanya vipimo vya kimatibabu na
klabu ya Leeds United. (AS)
Newcastle hawajaweka dau mpya ya
kumnunua kiungo wa kati wa Paraguay Miguel Almiron, 24, kutoka MLS
Atlanta United tangu ufa yao ya kwanza kukataliwa mwezi Desemba mwaka
jana. (Chronicle)
Chanzo BBC.

0 Maoni