Msafara wa wachezaji 18 na viongozi wa Klabu ya Sevilla FC umetua nchini usiku wa kumkia leo .
Sevilla
wametua nchini chini ya uratibu wa Kampuni ya Kubashiri Matokeo ya
SportPesa pamoja na Laliga. Sevilla wakiwa hapa nchini watacheza mchezo
mmoja wa kirafiki dhidi ya Simba kesho kutwa Alhamisi utakaopigwa Uwanja
wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mara
baada ya Sevilla kutua, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa,
Tarimba Abbas amesema kuwa anafurahia ujio wa Sevilla ambao utaongeza
utalii nchini.
Tarimba aliwatahadharisha Sevilla kwa kuwaambia kuwa wajiandae wanacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mabingwa wa Ligi Kuu Bara.
“Ninawaambia
kuwa jiandaeni kupambana na mabingwa wa ligi hapa nchini ambao ni
Simba.” Ni timu nzuri iliyojiandaa kuhakikisha inapata ushindi kutokana
na ubingwa walioupata,”amesema Tarimba.
Lakini
pia mara baada ya kuwasili nchini,kikosi hicho kililakiwa na burudani
sana kabisa kabisa kutoka kwa kundi la Ngoma za asili linaloongozwa na
Msanii mahiri wa kughani Mrisho Mpoto,ama kwa hakina walikunwa na
uchezaji ngoma na kujikuta nao wakiinuka kujimwaya mwaya kwa pamoja.













0 Maoni