Unordered List


KATIBU MKUU WA CCM DKT BASHIRU ALLY KAKURWA APOKEA KOMBE LA NDONDO CUP KUTOKA UVCCM TEMEKE

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Dkt Bashiru Ally Kakurwa akipokea Kombe la Ndondo Cup kutoka kwa timu ya Umoja wa Vijana wa CCM Temeke iliyoshinda Ubingwa huo 2019/2020

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Dkt Bashiru Ally Kakurwa tarehe 22/08/2019 amezungumza na Mabingwa wa Kombe la Ndondo Cup katika Ofisi ndongo za CCM Lumumba Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Vijana hao wa Team ya Umoja wa Vijana Wilaya ya Temeke pamoja na Wadau na Waandaaji wa kombe hilo,Amewataka wanamichezo kote nchini kuendelea kuitumia fursa hiyo Vizuri ili kufikia malengo waliyojiwekea.

Pia Dkt Bashiru amewataka Vijana wote nchini wenye nia ya kuwatumikia wananchi kushiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wenye uadilifu na Uzalendo kwa Taifa letu ili kuweza kusukuma gurudumu la maendeleo mbele.

Aidha amewataka Vijana kutotumika na Viongozi wanaowatumia nyakati za Shida za kiuchaguzi na kuwaasa kuendelea kuwa bega kwa bega na Viongozi waliopamoja nao wakati wa shida na raha, amesisitiza kuwa viongozi bora wa kuwachagua hawawezi kutokana na Chama kingine cha siasa bali Chama Cha Mapinduzi pekee, hivyo wakati wa Uchaguzi utakapofika wasifanye makosa

Pia Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Tanzania Ndg Galila R Wabanh’u (MNEC) alimshukuru Katibu Mkuu wa CCM kwa kukubali ombi la kutenga muda wa kupokea kombe hilo kutoka kwa mabingwa hao (UV-TEMEKE), aidha ameahidi kuwa UVCCM Taifa itaendelea kusaidia vijana nchi nzima kuibua vipaji vya michezo ambacho kitawasaidia katika maisha yao pamoja na kujenga umoja na mshikamano wa kitaifa.






Chapisha Maoni

0 Maoni