• UVCCM TAIFA

  SAUTI YA VIJANA,SAUTI YA UMMA.CCM MPYA,TANZANIA MPYA.

 • UVCCM TAIFA

  MWAKA MMOJA WA SERIKALI YA AWAMU YA TANO.

 • This is default featured slide 3 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

 • This is default featured slide 4 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

 • This is default featured slide 5 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

Alhamisi, 31 Oktoba 2013

Tunaweza kujitoa Jumuiya ya Africa Mashariki (Tanzania)


Mh, Samweli Sitta
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete
Serikali ya Tanzania imesema inatafakari ushiriki wake ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na inaweza kujitoa ndani ya Jumuiya hiyo iwapo itaendelea kutengwa katika baadhi ya vikao.
Aidha imesema Tanzania haitambui vikao vinavyofanywa na nchi tatu zilizopo ndani ya Jumuiya hiyo ambazo zimekuwa zikizitenga Tanzania na Burundi.
Waziri anayehusika na masuala ya Afrika Mashariki wa Tanzania Samwel Sitta ameliambia Bunge la Tanzania kuwa makubaliano ya vikao hivyo vinavyofanywa na nchi za Kenya, Rwanda na Uganda yatatekelezwa na nchi hizo zinazofanya vikao hivyo kwa sababu vinafanyika nje ya utaratibu wa mkataba wa jumuiya hiyo.
Katika mikutano iliyofanyika hivi karibuni Tanzania na Burundi hazikualikwa kwenye vikao hivyo.
Kwa mujibu wa Waziri Sitta mikutano ya wakuu wa nchi za Rwanda, Kenya na Uganda ambayo ilianza kwa kuitenga Tanzania ilifanyika Entebbe nchini Uganda mwezi Juni mwaka huu na kufuatiwa na mkutano wa pili uliofanyika Agosti mwaka huu huko Mombasa nchini Kenya ambapo nchi hizo tatu bila kuishirikisha Tanzania walizungumzia uanzishaji wa himaya moja ya forodha.
Mambo mengine waliyozungumza wakuu hao ilikuwa uanzishaji wa visa moja ya utalii kwa nchi zao na matumizi ya vitambulisho vya uraia ambavyo vitatumika kama hati za kusafiria miongoni mwa nchi hizo.
Aidha Waziri Sitta amesema ndani ya mikutano hiyo pia walizungumzia kuanzisha mchakato wa kuanzisha shirikisho la nchi hizo.
Tayari Tanzania imeanza mazungumzo na nchi za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kuangalia ni kwa namna gani zitaanzisha ushirikiano nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kama zinavyofanya nchi za Rwanda, Uganda na Kenya.
Share:

Jumatatu, 28 Oktoba 2013

Nafasi za Kazi Mwanza. (Job Oportunity)


Position:                                            IT Technician III (Training Institute,Mwanza and Head Office) – 3 Post
Reports to:                                        Head of Division
Contract type:                                   Contract for unspecified period of time
Location:                                           Bank of Tanzania Training Institute, Mwanza and Head Office, Dar es Salaam
Job Purpose:
To install, configure and maintain computers and peripherals in good working condition as well as to support   users of IT systems.
Primary Duties and Responsibilities:
a)   Installing, assembling and configuring computers, monitors, Laptops, Mobile devises and peripherals such sprinters, scanners and related hardware;
b)     Troubleshooting and repairing computer  systems hardware and software as well as other computer peripherals and ICT equipment;
c)      Troubleshooting and maintaining network infrastructure;
d)     Performing preventive  maintenance  of ICT equipment;
e)      Providing  support on applications such  as MS Office, MS Visio, MS Project, MS Exchange Outlook, MS SCCM and Lync, Desktop Clients and Agents and  Operating system issues to users;
f)       Providing support on antivirus and other anti-malware applications on desktops, laptops and mobile devices ;
g)     Performing other related duties as may be assigned.
Education/Professional Qualifications and Experience Required:
a)      Diploma in Electronics and Telecommunications Engineering, Computer Engineering or related fields;
b)     PC Technician certification will be an  added advantage;
c)      At least two (2) years of relevant working experience.

Share:

Alhamisi, 24 Oktoba 2013

Mgawanyiko wa EAC ni Tamaa au Migogoro tu.....!!!Bendera ya jumuiya ya Afrika mashariki
Serikali ya Tanzania imekosoa Muungano mpya wa hiari wa nchi za Kenya,Uganda na Rwanda ulioundwa hivi karibuni.
Serikali ya Tanzania imeuelezea kuwa unaenda kinyume na makubaliano katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Wakuu wa nchi za Kenya,Uganda na Rwanda walikutana hivi Karibuni nchini Uganda ambapo walikubaliana kuanzisha miradi ya pamoja ya kimaendeleo katika nchi zao hatua ambayo haijapokelewa vema na Serikali ya Tanzania
Hii ni ishara ya hivi karibuni kuwepo kwa mgawanyiko katika nchi wanachama katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Hii si mara ya kwanza kuzuka tofauti katika Jumuiya hii ambayo imeundwa ikiwa ni mara ya pili baada ya ile ya awali kuvunjika mwaka 1977 ,wakati huo ikiwa na wanachama watatu tu yaani Tanzania,Kenya na Uganda.
Mgogoro huu wa sasa inaelezwa kuwa chanzo chake ni mkutano wa pande tatu uliofanyika mapema mwezi July mwaka huu nchini Uganda ambapo nchi za Kenya,Uganda na Rwanda zilikubaliana kuungana katika kufanya miradi ya kimaendeleo ya pamoja ndani ya nchi zao,muungano ambao unaonekana kuitenga Tanzania,huku Burundi hivi karibuni nayo ikijiunga na Muuungano huo na kuufanya kuwa wa nchi nne.
Tanzania inasisitiza kuwa kulipaswa kuwepo na mazungumzo na maafikiano miongoni mwa nchi wanachama kabla ya kuanza utekelezaji wake.
Katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya ushirikiano wa Afrika Mashariki imetaja kuwa nchi hizo zimekiuka makubaliano yaliyoko kwenye mkataba wa jumuiya hiyo.
Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yenye makao yake Makuu mjini Arusha haijasema lolote tangu kuanza Muungano huo wa nchi tatu na wala haijajibu malalamiko hayo ya Serikali ya Tanzania.
Share:

Jumanne, 22 Oktoba 2013

Faida kedekede na Changamoto za Treni ya,Mwakyembe

 
Mmoja wa wanafunzi (kulia) akionekana kufurahia usafiri wa treni. Picha na Zakaria Osanga  

 Terehe 29 Oktoba, mwaka huu treni ya usafiri Jijini Dar es Salaam maarufu kama treni ya Mwakyembe inatimiza mwaka mmoja wa kutoa huduma hiyo.

Swali kuu ni je, uwepo wa huduma hii umesaidia kuondoa au kupunguza shida ya usafiri?
Wasemavyo watumiaji
Saa 11 kamili jioni, jijini Dar es Salaam, Saida Adam mwanafunzi wa kidato cha kwanza, Shule ya Sekondari Zanaki na Mery Peter (darasa la tatu) Shule ya Msingi Kisutu wanashuka kwenye treni hapa Tabata Relini.
Hakuna aliyewasukuma kuwazuia wakati wa kupanda wala aliyewazuia wasikae kwenye viti kwenye usafiri huo.
Maumbo yao madogo na wakati mwingine ubabe wa makondakta vingewapa wakati mgumu kuhimili mikiki ya abiria waliochoka wanaowania kupanda daladala.
Watoto hawa ni miongoni mwa abiria wengine karibu 14,000 ambao wanafanya safari zao kwa siku kwa chombo hicho.
Saada na Mery wanaelezea tamu ya usafiri huo ambao unatimiza mwaka mmoja tangu Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe alipozindua rasmi usafiri huo.
“Ni usafiri rahisi kwa sababu hauna foleni, kwa hiyo ninawahi kufika nyumbani, sinyanyaswi na nauli yake ni ndogo (Sh100)” anasema Saada.
“Kwa mimi kama ningetumia daladala ningetumia hadi saa tatu ili nifike nyumbani” anasema Mery ambaye anamaanisha kuwa ‘treni ya Mwakyembe’ imewarahisishia kazi.
Kwa mujibu wa takwimu za Dk Mwakyembe, abiria 9000 wanasafiri kati ya Pugu Mwakanga hadi Kurasini kupitia Shirika la Reli kati ya Tanzania na Zambia (Tazara) na 5000 wanasafiri kati ya Ubungo na Stesheni kwa kampuni ya reli(TRL).
Halima Mussa ni mmoja wa abiria hao anasema “Usafiri huu ni mzuri, huduma zao nzuri, wafanyakazi ni wastaarabu nauli yao nzuri (Sh400), na unapunguza msongamano ambao tungeupata kwenye daladala,” anasema.
Furaha ya Halima inaleta kilio kisichokuwa na machozi kwa madereva, makondakta na wamiliki wa daladala.

Emmanuel Peter anamiliki daladala inayofanya safari zake kati ya Ubungo na Mnazi Mmoja kupitia barabara ya Mandela.
Ujio wa treni hiyo ya Mwakyembe uliyumbisha biashara yake na makusanyo aliyokuwa akiyapata kwa siku yalipungua.
“Kuna wakati tulikuwa tukigombana na madereva na makondakta kwa sababu hesabu ya fedha ilikuwa haitoshi,” anasema Peter.
Peter anasema abiria wanaotumia daladala walipungua japo hesabu wanayoitaka ilikuwa inafika lakini ni tofauti na ilivyokuwa hapo awali kabla Mwakyembe hajaja.
Huko Mabibo ambapo treni hiyo ina kituo ndipo kuna mapinduzi makubwa, yanawapa changamoto wenye daladala.
Kondakta wa daladala inayofanya safari kati ya Mabibo na Kariakoo, Ali Said anasema hali ya kibiashara imeshuka tangu usafiri huo wa garimoshi uchukue nafasi.
“Kipindi cha nyuma ulikuwa huwezi kukuta magari yamepangana foleni hivi muda kama huu wa asubuhi” anasema Said akionyesha daladala zilizopanga foleni kusubiri abiria wa kwenda Posta na Kariakoo.
Anaongeza kuwa abiria wanaowapata ni wale wa maeneo ya Manzese na Magomeni ambapo reli haipiti.
Kuhusu kipato, Said anakiri kuwa kimeshuka japo hataki kuweka wazi kimeshuka kwa kiasi gani.
Kondakta huyo anasema magari yanayofanya safari za Mabibo- Kivukoni yamepungua tangu treni hiyo ilipoanza safari zake Oktoba mwaka jana.
Hata hivyo wadau wengine wa daladala inapopita reli ya Tazara wanasema wao hajaathirika sana.
Dereva wa daladala inayofanya safari kati ya Kigogo na Kariakoo, Mohamed Ramadhan anasema hakuna tofauti tangu treni ilipoanza safari zake kutoka Pugu hadi Kurasini.

“Saa 12 asubuhi ikibeba watu kuna wengine wanaoenda sehemu ambazo haipiti kwa hiyo tunawachukua sisi,” anasema Ramadhan.
“Kwa sababu inapita sehemu za ndani ambapo sisi hatupiti inachukua abiria wa huko,” anaongeza Ramadhani.
Katika mwaka mmoja imesaidia mengi, mmoja wa abiria wa usafiri huo wa Mwakyembe, Athuman Mrisho anataka idadi ya mabehewa iongezwe kutoka 8 ya sasa hadi 12.
Mrisho anataka ifanye kazi pia siku ya jumapili ambapo anapendekeza angalau mabehewa matatu yatumike kwa siku hiyo.
Waziri Mwakyembe wakati akiwasilisha bajeti ya wizara yake bungeni alisema abiria 14,000 wanaosafiri kwa treni kwa siku, wangehitaji mabasi zaidi ya 467 yenye uwezo wa kuchukua abiria 30 kila moja.
Moja ya mahitaji yanayosubiriwa na usafiri huo ni pale itakapoanzisha usafiri wa kwenda Gongo la Mboto ambapo shida ya usafiri inazidi kuongezeka kila siku.
Huduma hiyo ya treni ilizinduliwa na kuanza kazi rasmi Oktoba 29 mwaka jana, huku wengi wa wananchi wakiwa na matumaini kuwa ingesaidia kupambana na tatizo la usafiri linalonekana kusumbua katika Jiji la Dar es Salaam.
Wananchi wengi waliongea na mwandishi wa makala hii wameshauri Serikali kuangalia namna ya kuiboresha huduma hii ambayo inaonekana wazi kwamba ikiboreshwa inaweza kufanya usafiri kuwa wa uhakika zaidi ya ilivyo sasa.
Aidha wameishauri Serikali kuangalia namna ya kutoa huduma za usafiri wa treni wa ndani ya mikoa na mikoa jirani kwa kadri inavyowezekana ili kuharakisha maendeleo nchini.

 Na Zakaria Osanga, Mwananchi
Share:

MAGAZETI YA LEO JUMANNE

Share:

Jumatatu, 21 Oktoba 2013

CCM lazima Ichukue Dola kwa Kishindo 2015
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepanga na kuendesha mafunzo kwa makatibu wake wa Mikoa na Wilaya zote hapa nchini. Mafunzo hayo pia yatajumuisha ushiriki wa wenyeviti wa wilaya na baadhi ya watendaji na watumishi wa Makao Makuu na ngazi nyingine zisizo rasmi za Chama Cha Mapinduzi.

Mafunzo hayo yameanza rasmi leo ambapo Makamu Mwenyekiti Taifa ambae pia ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mheshimiwa Dr Ali Mohamed Shein alifanya ufunguzi wa mafunzo hayo katika ukumbi wa Makao Makuu ya Chama maarufu kama whitehouse jijini Dodoma.


Katika Hotuba hiyo Makamu Mwenyekiti alisisitiza kuwa mafunzo hayo ni vuguvugu za kuelekea 2014/2015 na kwamba watendaji wa chama watambue kuwa sasa wanaingia rasmi katika mbio na heka heka za Uchaguzi. Sehemu ya nukuu ya hotuba hiyo inasema


"..Napenda ieleweke kwamba, miongoni mwa malengo ya mafunzo haya ni kuimarisha uhai wa Chama chetu wakati huu tunapoelekea katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Tanzania Bara hapo mwakani pamoja na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.


Nina imani kubwa kuwa mafunzo haya yatakuwa na manufaa makubwa kwa washiriki wote na yataleta tija katika utendaji wa majukumu yenu. Tunategemea baada ya mafunzo haya, tutashuhudia na kuona vugu vugu la kuimarika kwa shughuli za chama chetu nchi nzima. Hali hiyo, lazima iende sambamba na maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2014 ambapo kama kawaida yetu ushindi ni lazima.."

Pamoja na ufunguzi wa mafunzo, Makamu Mwenyekiti ameipongeza tume ya mabadiliko ya Katiba kwa kazi nzuri waliyoifanya na amebeza propaganda zilizoenezwa kuwa Chama Cha Mapinduzi kilihodhi mchakato wa ukusanyaji wa maoni na kwamba Chama Cha Mapinduzi kinawahakikishia watanzania kuwa kitaheshimu maoni ya watanzania wakati wa kura za maoni (referendum) wakati ukifika.

Katika kuhitimisha Dr Shein akahimiza Umoja ndani ya Chama na kuwakumbusha watendaji juu ya Uadilifu katika utendaji wao. Na kusisitiza kuwa Chama hakitashindwa kuwachukulia hatua wale wote wataogundulika kutokuwa na Uadilifu na kusababisha Uimara wa Chama kulega lega.

Share:

Nikweli wanajeshi wa Kenya walipora Westgate......!!!!?
Mmoja wa wanamgambo wa Al Shabaab wanaosemekana kuuawa kwa shambulizi la Westgate


Picha za wanajeshi wa Kenya waliokwenda katika jumba la Westgate katika juhudi za uokozi na kisha baadaye kuonekena kwenye kamera za CCTV wakiondoka na mifuko ya plasitiki yenye bidhaa za madukani, bila shaka zimewashangaza wengi
.
Picha hizo mwanzo zimeonyesha wanajeshi wakiingia ndani ya jengo hilo wakiwa wamebeba silaha kukabiliana na wanamgambo walioshambulia jengo hilo wiki nne zilizopita na baadaye wakitoka wakiwa wamebeba mifuko hiyo wakiwa na silaha zao kwa wakati mmoja.
Hata hivyo haijulikani walichokuwa wamekibeba kwenye mifuko hiyo .
Pamoja na picha za wanajeshi wakiwa wamebeba mifuko, pia kulikuwa na picha zengine zilizoonyesha mashine ya pesa zikiwa zimeporwa ndani ya mikahawa huku picha za alama za risasi kwenye maeneo ya kuhifadhia pesa, pia zikionekana
.
Inaarifiwa ilikuwa jaribio ya kufungua hifadhi hizo ambalo halikufanikiwa.
Madai haya ya wanajeshi kufanya uporaji wa maduka katika jingo hilo, yalikanushwa vikali na jeshi la Kenya kiasi cha kutaka hatua kuchukuliwa dhidi ya waliokuwa wanatoa madai hayo, lakini haijulikani jibu lao litakuwa nini hasa kwa picha hizo za CCTV zilizoonyesha wanajeshi hao wakifanya uporaji.
Wamiliki wa maduka waliorejea kwenye maduka yao baada ya shambulizi , walidai kuwa maduka yao yaliporwa ingawa jeshi lilikanusha madai hayo baadhi ya taarifa zikisema kuwa ilikuwa njama ya wafanyabiashara kudai fidia kwa mali zao zilizoharibika
.
Sio wanajeshi pekee waliotuhumiwa kwa uporaji, kwani polisi mmoja naye alifikishwa mahakamani kwa kosa la uporaji baada ya kupatikana na pochi la mtu liliokuwa na damu.
Wagambo wa Al Shabaab waliteka nyara jengo la Westgate kwa siku nne na kusababisha vifo vya watu 60 pamoja na kuwajeruhi zaidi ya watu miamoja.
Share:

Makamu wa Rais Dkt Bilal afungua mkutano wa Mabunge ya SADC mjini Arusha leo

Makamu wa Rais Dkt Bilal afungua mkutano wa Mabunge ya SADC mjini Arusha leo

Imetumwa kwenye Jamii
vice_7d4d2.jpg
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua mkutano wa siku 11 wa 34 kwa Mabunge ya Nchi wanachama wa Jumuiya ya SADC katika ukumbi wa A I C C mjini Arusha leo 20 Octoba 2013.
lema_8d979.jpg
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mbunge wa Arusha mjini Mhe. Godbles Lema nje ya ukumbi wa mikutano wa A I C C Arusha, Baada ya kufungua mkutano wa siku 11 wa 34 kwa Mabunge ya Nchi wanachama wa Jumuiya ya SADC katika ukumbi wa A I C C mjini Arusha leo 20 Octoba 2013. Kushoto Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nasari.
pindu_29aa4.jpg
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Pandu Ameir kificho kabla ya kufungua mkutano wa siku 11 wa 34 kwa Mabunge ya Nchi wanachama wa Jumuiya ya SADC leo Octoba 20, 2013 katika ukumbi wa A I C C mjini Arusha.
speaker_2989f.jpg
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia vikundi vya sanaa vya ngoma za aina mbalimbali alipowasili katika Jengo la Ukumbi wa mikutano A I C C mjini Arusha kwa ajili ya kufungua mkutano wa siku 11 wa 34 kwa Mabunge ya Nchi wanachama wa Jumuiya ya SADC leo Octoba 20, 2013.
(Picha na OMR) (P.T)

Mpira umemalizika, Simba SC 3 -3 Young Africans

Imetumwa kwenye Michezo
4_6_55973.jpg
Ngassa dkk 14, Kiiza dkk 35, 45
Mombeki dkk 55, Owino dkk 57, Kaze dkk 84(P.T)

Share:

BOKO HARAMU WAUA MADEREVA 19 NIGERIA


131015124213_nigeria_bokoharam_304x171_afp_acd2c.jpg
Wanamgambo waliokuwa wamevaa nguo za kijeshi, wamewaua watu 19 katika kuzuizi cha barabarani walichokuwa wameweka kukagua magari katika jimbo la Borno.
130920090824_nigeria_304x171_ap_13bd5.jpg
Mabaki ya magari ya madereva waliouawa na Boko Haram
Wanaume hao waliokuwa wamejihami , waliwasimamisha madereva na kuwaamrisha kuondoka kutoka katika magari yao kabla ya kuwapiga risasi na kuwaua.
Walioshuhudia tukio hilo waliambia BBC kuwa wanaume hao walikuwa wanachama wa Boko Haram, ingawa kundi hilo bado halijatamka chochote kuhusu mauaji hayo.
Jimbo hilo la Kaskazini mwa Nigeria liko chini ya sharia ya hali ya hatari, huku Boko Haram wakiwa vitani na serikali kutaka utawala wa kiisilamu.(P.T)
Kundi hilo huwalenga raia na wanajeshi kwa mashambulizi ikiwemo shule na makabiliano ya mara kwa mara na jeshi la taifa.
Shambulizi la hivi karibuni, lilifanyika Jumapili, asubuhi karibu na mji wa Logumani, ambao hauko mbali sana na mpaka na Cameroon.
Walionusurika shambulizi hilo walisema kuwa washambuliaji walivaa nguo za jeshi na walikuwa wanaendesha pikipiki kabla ya kuwashambulia waathiriwa.
"Takriban wanaume 9 walituamuru kuondoka kwenye magari yeu na kulala chini,'' alisema mwanamume
"Waliwaua watu 5 kwa kuwapiga risasi na kasha kuwanyonga wengine 14 kabla ya mtu mmoja kuwapigia simu na kuwambia kuwa wanjeshi wanakuja.''
Alisema washambuliaji baadaye walitoroka na kujificha msituni kwa pikipiki zao.
Manusura mwingine alisema kuwa alisikia mtu aliyekuwa karibu naye akiuawa kwa kisu. Alisema ana uhakika kuwa washambuliaji walikuwa Boko Haram kwa sababu ya kuwa na ndevu.
Mwandishi wa BBC Tomi Oladipo alisema kuwa ni jambo la kawida kwa polisi kuweka vizuizi barabarani hasa katika maeneo yenye misukosuko na huenda washambuliaji waliiga mbinu hioyo ya jeshi ili kuwanasa waathiriwa. I,
Boko Haram limezua mgogoro mkubwa wa kisiasa Nigeria tangu mwaka 2009, nia yao kuu ikiwa kuunda utawala wa kiisilamu, hasa katika maeneo ya kaskazini mwa nchi
Kundi hilo limelaumiwa kwa mashambulizi kadhaa ambao yamesababisha takribna vifo 2,000 tangu mwka 2011.
Share:

MAGAZETI YA LEO JUMATATU

DSC 0057 aae29
DSC 0058 6a210
DSC 0059 42743
DSC 0060 14b36
DSC 0061 32764
Share:

Jumapili, 20 Oktoba 2013

NAFASI MPYA ZA KAZI Geita gold mine leo tr, 20/10/2013 deadline 03/11/2013

 
 Geita Open pit operation

POSTS--- DRIVER- (20)POSTS INCLUDING A VALID NEW DRIVING LICENCE- (VETA/NIT CERTIFICATE IS AN ADDED ADVANTAGE (2)DRILLERS---(12)POSTS (3)MACHENERY OPERATORS 10 POSTS!!!!)(DOZER,EXCAVATOR,WHE ELLOADER,DUMPTRUCK,MOTOR GRADER,CRANE. (4)BOILER MAKERS ---(8 POSTS)....(5)PROCUREMENT OFFICERS(6 POSTS).... (7)-SECURITY GUARDS--(40 POSTS)....(8-MINING ENGINEERS (4 POSTS).... (9)INFORMATION TECHNOLOGY MANAGERS (4 POSTS) DEADLINE YA KU APPLY NI NOVEMBER 3, FOWARD YOUR CV TO ......HUMAN RESOURCES MANAGER GEITA GOLD MINE P.O. BOX 532 GEITA-MWANZA. Email. jobs@geitagold.com OR geitarecruitment@rocketmail.co m

Haya vijana tuchangamkie Hizi kazi kwani hizi ndo Fulsa zenyewe kwa vijana wetu kwakitanzania chini ya uongozi wa CCM, na Sera ya Uwekezaji.

 Ariel View of Geita Mine
Share:

Ijumaa, 18 Oktoba 2013

RAIS KIKWETE MKOA WA NJOMBE

jk_njombe_c4f24.jpg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili mjini Njombe jana jioni, Alhamisi, Oktoba 17, 2013, kuanza ziara ya wiki moja kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Njombe.
Miongoni mwa shughuli kubwa ambazo Rais Kikwete atazifanya katika ziara hiyo, ya kwake ya kwanza tokea Njombe kutangaza kuwa Mkoa, ni kuuzindua rasmi Mkoa huo.
Katika siku yake ya kwanza leo, Ijumaa, Oktoba 18, 2013, mbali na kuzindua Mkoa wa Njombe pia atazindua Kiwanda cha Chai katika eneo la Ikanga na kuzungumza na wananchi.
Katika ziara hiyo ambako Rais Kikwete atatembelea wilaya zote za mkoa huo ambazo ni Njombe, Wanging'ombe, Ludewa na Makete, pia atazindua Chuo cha Veta cha Mkoa.
Aidha, Rais atatembelea na kupata taarifa kuhusu maendeleo ya mradi wa chuma wa Liganga.(P.T)
Share:

Alhamisi, 17 Oktoba 2013

serikali ya obama yapata ahueni

us f62db
Baraza la Congress nchini Marekani, limepitisha mswaada utakaowezesha serikali kuendelea ma majukumu yake ya kifedha na kuongeza muda wake wa kulipa madeni yanayoikabili. (HM)

Hatua hii imekuja masaa kadhaa kabla ya serikali kutumbukia kwenye mkwamo wa kifedha.

Baraza la senate lenye waakilishi wengi wa Democtrats lilishinda kura ya mswaada huo kwa kura 81 dhidi ya 18
Mswaada ulipitishwa kwa kura 285 dhidi ya 144 katika bunge la waakilishi ambapo wabunge wa Republican waliunga mkono mswaada huo shingo upande.
Afueni hii kwa serikali ya Rais Barack Obama imekuja masaa kadhaa kabla ya makataa ya kuongeza kiwango cha deni la serikali hadi dola trilioni 16.7.
Mswaada huo sasa utawezesha serikali kuendelea na majukumu yake ya kifedha na hata kuomba pesa zaidi kutoka katika hazina ya serikali hadi Februari tarehe saba.
Pia itawezesha serikali kupata pesa hadi Januari kumi na tano na kufungua mashirika ya kifedha katika majimbo na kuwaresha kazini maelfu ya wafanyakazi wa serikali.
Ikulu ya White house sasa imewataka wafanyakazi wa umma kurejea kazini leo.
Mswaada huo hata hivyo ni afueni ya muda na sio suluhu kwa matatizo ya bajeti ya serikali ambayo yaliwagawanya wanasiasa wa Republican na Democrats.
Baada ya mswaada kupitishwa, Rais Barack Obama aliwaambia waandishi wa habari kuwa atasaini mswaada huo na kuufanya sheria. Chanzo: voaswahili
Share:

Jumapili, 13 Oktoba 2013

NAPE ASHIRIKI MAZISHI YA TAMBALIZENI


 • Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ameongoza mamia ya wakazi wa Dar Es Salaam na mkoa wa Pwani katika mazishi ya Kada na Mshairi maarufu wa CCM salum Tambalizeni yaliyofanyika Marumbo Kisarawe.
 • Pia atoa heshima za mwisho kwa Kada wa CCM na kiongozi wa wazazi Tawi la Mbuyuni kata ya Kigogo,Marehemu Clemence Ndaghala aliyefariki tarehe 10 Oktoba katika hospitali ya muhimbili baada ya kuugua kwa muda mfupi.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kisarawe Ndugu Tatu Kana leo Marumbo Kisarawe kabla ya mazishi ya Kada na Mshahiri wa CCM Salum Tambalizeni.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitoa salaam za pole kwa wafiwa kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi na salaam za Mwenyekiti wa CCM Taifa, ambapo alimwelezea Tambalizeni kuwa alikuwa mtu wa kupenda kusaidia watu na kushiriki kwenye masuala ya maendeleo ya watu waliomzunguka,aliendelea kusema si rahisi pengo lake kuzibika.
   Mwili wa marehemu Salum Tambalizeni ukipelekwa makaburini.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kutia udongo kwenye kaburi la Marehemu Salu Tambalizeni.
  Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Ndugu Sixts Mapunda akishiriki kutia udongo wakati wa mazishi ya Salum Tambalizeni yaliyofanyika Marumbo Kisarawe.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi  Nape Nnauye akiwa pamoja na wakazi wa kata ya Kigogo ambapo alishiriki kutoa heshima ya mwisho kwa Marehemu Clemence Ndaghala aliyefariki tarehe 10 Oktoba na kusafirishwa leo kuelekea Ifakara kwa mazishi.
 Ndugu,Jamaa na Majirani wa Clemence Ndaghala wakipokea neno takatifu kabla ya kuanza kutoa heshima za mwisho kwa mpendwa wao Clemence Ndaghala aliyefariki tarehe 10 Ocktoba katika hospitali ya Muhimbili.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Clemence Ndaghala aliyefariki tarehe 10 Oktoba kwenye hospitali ya Muhimbili jijini Dar es salaam.
Share:

Ijumaa, 11 Oktoba 2013

SASA HOTUBA ZA HAYATI BABA WA TAIFA MWL JK NYERERE KUPATIKANA KWENYE SIMU YA KIGANJAKANI

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiki akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa huduma ya kupata hotuba za Marehemu baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika kwenye hotel ya Double Tree jana. Ili kuweza kupata hotuba za maneno na picha za video unatakiwa kutuma neno Hotuba kwenda namba 15678, pia unaweza kupata huduma hiyo kwa kutumia www.simu.tv/nyerere mobile tv. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Push Media Mobile Freddie Manento
Share:

Alhamisi, 10 Oktoba 2013

MULUGO ATAKA WALIOKOSA MIKOPO KUJISOMESHA


148 Philipo-Mulugo1 57d1b
Na Gladness Theonest
Serikali imewataka wanafunzi waliokosa mikopo kwa ajili ya masomo vyuo vikuu kurudi nyumbani na ikiwezekana wakauze viwanja au ng'ombe ili waweze kujisomesha kwani bajeti iliyopo haitoshi.Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip Mulugo,wakati akizungumza na wanafunzi waliokosa mikopo ambapo kwa takriban wiki nzima wamepiga kambi wizarani hapo.(hd)
"Kasungura kadogo na mkumbuke kuwa mkopo ni kuomba kuna kupata na kukosa...hivyo wale waliokosa na walikuwa na vigezo watafute watu wengine wenye uwezo wawasomeshe kwa mwaka mmoja na unaofuata watume tena maombi," alisema.
Alisema kilio chao amekisikia na leo atazungumza na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuhusiana na malalamiko yao ambapo suala hilo litapelekwa Bungeni ili kujadiliwa.
"Kama Bunge litaamua kupunguza fedha kutoka kwenye bajeti zingine ili kusomesha wanafunzi hao. Bunge litaamua kwani Serikali ina nia nzuri sana kwani hadi sasa imetoa trilioni 1.5, lakini ndugu zenu hawarudishi," alisema.
Alitaja sababu nyingine ya wanafunzi kukosa mikopo ni Serikali kuangalia uhitaji, kwani kuna masomo maalumu walilenga hasa fani zenye upungufu wa wataalamu.
Alitaja fani hizo kuwa ni ualimu, udaktari na wahandisi. Alitaja sababu nyingine za wanafunzi kukosa mikopo hiyo ni waombaji kukosea majina na vitu vingine vidogo vidogo na walipotangaziwa kwenye vyombo vya habari warudi kurekebisha fomu zao hawakufanya hivyo.
Alisema waliokosea kujaza fomu hizo walikuwa 6,000 lakini waliorudi kufanya marekebisho walikuwa ni 3,000 na wengine 2,000 walikuwa na vigezo lakini wamekosa kutokana na sungura kuwa mdogo (bajeti).
Wanafunzi waliokosa mikopo walisema kama wenzao wameweza kupata mikopo kwa asilimia 100 basi waangalie namna ya kugawana ili wote waweze kupata
Share on facebook:CHANZO MAJIRA
Share:

Taylor kutumikia kifungo Uingereza

_60577231_jex_1420959_de27-1_537c3.jpg
Aliyekuwa Rais wa Liberia Charles Taylor atatumikia kifungo chake cha miaka 50 jela nchini Uingereza baada ya kupatikana na hatia ya uhalifu wa kivita.
Haya ameyasema waziri wa sheria nchini Uingereza Jeremy Wright.
Sweden na Rwanda pia zilikuwa zimeomba kumfunga jela Taylor katika ardhi yao baada ya rufaa yake kukataliwa na mahakama mwezi jana.(P.T)
Taylor alihukumiwa kifungo cha miaka 50 jela na mahakama maalum ya Umoja wa Mataifa kuhusu Sierra Leone, mjini Hague.
Iliamua kuwa makosa dhidi yake yalithibtishwa bila tashwishi.
Alihukumiwa jela mwaka 2012 kwa kuwasidia waasi waliofanya maasi makubwa dhidi ya watu wa Sierra Leone wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.
Taylor, mwenye umri wa miaka 65, alipatikana na hatia ya kuwapa waasi wa Revolutionary United Front silaha na wao wakimpa almasi kutoka Sierra Leone.
Share:

Ijumaa, 4 Oktoba 2013

NAPE AZUNGUMZIA MSIMAMO WA CCM

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari leo katika Ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM-Lumumba Dar es Salaam. Alikuwa akitoa ufafanuzi kuhusu masuala yahusuyo Mchakato wa Katiba mpya na kusema "tunaheshimu tume,tunaimani nayo na tunaahidi ushirikiano wa kutosha katika mchakato wa Katiba".
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Gadget

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu